Hii hapa Television ya kumiliki kulingana na kipato chako

Hii hapa Television ya kumiliki kulingana na kipato chako

Kila mtu anapenda kumiliki kitu kizuri ila baadhi kipato hakiruhusu, hii imepelekea kuwepo kwa bidhaa za kila aina sokoni ili kubeba pesa yoyote mteja aliyonayo. Kwa upande wa TV zipo kampuni nyingi sana na hapa nazigawa kwenye makundi matatu

1. Samsung LG SONY Panasonic
2. TCL Hisense Haier
3. Alitop Aborder Ailyons Solarmax Skyworth Mr.UK Mewe Boss e.t.c

Kutoka kundi namba moja TV ambazo zimezoeleka sana ni LG na Samsung, tofauti ya hawa wawili LG anakupa picha kali (real 4K) wakati Samsung anakupa picha kali pamoja na frame kali kuliko frame ya LG. LG anakupa durability na kioo chake ni kigumu kupasuka kuliko Samsung.

LG wanakupa series 4 ambazo ni (UHD NANOCELL QNED OLED) Samsung wao wana (UHD QLED OLED)

Bei zake zinapanda kulingana na latest series, kumiliki TV za kundi hili lazima uwe una pesa kulingana na series unayotaka pamoja na inches ngapi unahitaji na ndio TV zenye bei kubwa zaidi sokoni.

Namba mbili tukianza na TCL ni TV nzuri ambayo kama unapenda kitu kizuri na umeshindwa kufika bei ya hapo juu, TCL wanakupa picha nzuri pia inadumu ukiweka ndani ni mkataba.

Tukija kwenye hisense wenyewe wana series za bei ndogo na kubwa, hawa jamaa wana TV nzuri kulingana na bei zao ila quality yake haiwafikii hao wazee hapo juu, pia ndio TV ambazo zinauza sana sokoni kwa sasa kutokana na jina lakini pia bei zao zinaendana na watu wa uchumi wa kati, hawa jamaa baadhi ya series zao zinarudi sana kwa fundi ila ukiotea ni mkataba.

Haier wenyewe wamekuja karibuni kwenye soko la Tanzania na wanafanya vizuri, bei zao zipo chini kidogo ya Hisense, ukikosa pesa ya kununua hisense basi kimbilia hapa kabla hujafika namba tatu kwa wachina wenyewe.

Kundi namba tatu nimeweka kampuni za kichina zilizojaa sokoni, hawa wameamua kumuuliza mteja ana bei gani kisha watengeneze bidhaa, kwa hili kundi TV yenye picha nzuri ni Alitop na Skyworth lakini pia bei zao ni nzuri unaweza kumiliki 43" below 450k price; Aborder wanakupa durability nzuri pia.

Uliza swali lolote kwenye coments kulingana na mada, ukitaka kujua bei weka kampuni gani na inches ngapi, lakini pia series kama haufahamu uliza nitajibu.
Ciao

Goodvision 43" picha nzuri uimara kama wote​

 
Hata siku moja msijidanganye kwenye ulimwengu wa electronics especial TV's kwasasa mkamlinganisha Samsung na hao wengine. LG ni wabovu sana tena kwenye vioo.
Mkuu labda LG fake
Ninayo huu mwaka wa 3 na haina tatizo lolote ni
50inch tena bei ilikuwa rahisi sana kwa ulaya
Naona huko wanawaingizia fake nyingi sana
20241008_184613~2.jpg
 
Kwa hiyo bei ungeongeza 40k ungepata Alitop 43" ina kioo kizuri sana kwa hizi kampuni za kichina
Wenge kaka.ndo maana najuta.alafu hivi wale wauzaji uwa wana kitu gani wanaweka.
Ukion TV ipo dukani.picha inaonesha clear kabisa mpaka unasema hii si ndo TV.mama wee.ibebe sasa .mawingu sio mwaingu,ukungu sio ukungu.au wana kiini macho?
 
Wenge kaka.ndo maana najuta.alafu hivi wale wauzaji uwa wana kitu gani wanaweka.
Ukion TV ipo dukani.picha inaonesha clear kabisa mpaka unasema hii si ndo TV.mama wee.ibebe sasa .mawingu sio mwaingu,ukungu sio ukungu.au wana kiini macho?
Inategemea wana play kutumia source gani, kwa mfano TV zenye 4K mtu akiweka content ya 4k itaonekana vizuri ila ukifika nyumbani ukaunganisha na azam wao hawana content yenye 4k hapo lazima uone mawingu
 
Kwa hizi za kichina TV nyingi usiwe na mpango wa kuishi nayo miaka mitatu apo utawi

Nimesikia kuwa Hisense huwa zinatoka sana mistari hasa kuanzia inch 43 kwenda juu
Ninayo ni mwaka Sasa,na imepitia changamoto zote mpaka zile za wanadamu wenye" fungu la kukosa" mpaka sasa ninayo inadunda, unajua" fungu la kukosa" waliniibia hadi remote ya Tv yenyewe, remote ya king'amuzi Na redio lakini nadunda tu kudaadeki.
 
Inategemea wana play kutumia source gani, kwa mfano TV zenye 4K mtu akiweka content ya 4k itaonekana vizuri ila ukifika nyumbani ukaunganisha na azam wao hawana content yenye 4k hapo lazima uone mawingu
Ngoja nipambane nichukue Samsung. Mimi napenda TV sana.
Hela za kununua magari hatuna. Hata TV nzuri zitushinde?
 
Back
Top Bottom