Hii harusi ni zaidi ya kufuru, kuna watu wana pesa na wanajua kuzitumia

Hii harusi ni zaidi ya kufuru, kuna watu wana pesa na wanajua kuzitumia

Half american

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
38,283
Reaction score
97,793

Baada ya Rihanna na Katy Perry na Pitbull, Justin Bieber alipwa shilingi bilioni 26.4($10 mil ) kutumbuiza katika shamrashamra za harusi ya mtoto wa tajiri namba moja India na bara la Asia kwa ujumla

Bieber tayari ametumbuiza tarehe 5 July hii katika sherehe hiyo ya ndugu wa familia za pande zote na marafiki kujumuika(sangeet), pia mastaa wa Bollywood, Salman Khan, Alia Bhatt na Ranveer sigh nao walitumbuiza.

Ndoa rasmi itafungwa tarehe 12 July hii kisha reception kufanyika tarehe 14 mwezi huu ambapo mabilionea, viongozi wa nchi mbalimali na mastaa wa bollywood wanatarajiwa kuhudhuria

Awali, mwezi March mwaka huu katika uzinduzi wa siku tatu wa sherehe za ndoa/harusi hiyo Rihanna alitumbuiza baada ya kulipwa mabilioni ya shilingi, wageni waalikwa walikuwa zaidi ya 1,000

Kisha mwezi May mwaka huu katika muendelezo wa siku nyingine tatu za kusherehekea harusi hiyo, wageni waalikwa wakiwemo mastaa wa Bollywood walisafirishwa kwa Yatch ya kifahari kutoka nchini Italy kwenda Ufaransa ambapo Katy Perry na Pitbull walitumbuiza mbele ya waalikwa

Pamoja na hayo familia hiyo ya kitajiri ilitenga sherehe maalum ya kulisha chakula watu zaidi ya 51,000 wa hali ya chini inapokea familia ya bilionea husika kiasili

KUHUSU BWANA HARUSI PICHANI

Ana miaka 29, ni mtoto wa mwisho wa bilionea namba moja bara la Asia. bwana harusi huyo ni mhitimu wa chuo kikuu cha Brown nchini Marekani, yupo kwenye bodi ya wakurugenzi katika makampuni mbalimbali ya baba yake, lakini pia bwana harusi huyo yeye mwenyewe tayari pia amewekeza biashara zake binafsi katika sekta ya nishati

KUHUSU BIBI HARUSI PICHANI

Ana miaka 29, ni mhitimu wa chuo kikuu cha New York, Marekani, ni dancer professional aliyefunzwa kwa miaka kadhaa katika sanaa za kihindi, ni mfanyabiashara lakini pia wazazi wake nao ni matajiri waliowekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya. Bibi harusi huyo pia yupo kwenye bodi ya wakurugenzi katika kampuni zinazomilikiwa na wazazi wake

Maharusi hao watarajiwa wanafahamiana muda mrefu, Walichumbiana mwaka jana

Harusi hii itakula pesa nyingi ila pia mwaka 2018 bilionea husika katika harusi ya mwanae wa kike alipoolewa takribani dola milioni $100 zilitumika.

Baba wa bwanaharusi ni Mukesh Ambani ambaye ni bilionea namba moja India na Asia na kidunia anashika nafasi ya tisa kwa utajiri wa dola za Kimarekani billoni $116 alionao.
FB_IMG_17204566428796449.jpg
 
Hayo matumizi ya pesa kama mimi mzazi nisingetumia kwenye harusi ya bonge nyanya kama hilo!

Muda wowote huyo mwanamke ataveshwa nje ilibidi kwanza aanze na kumnunulia zana za kupiga tizi kuondoa minyama uzembe hiyo iliyokusanyana mwilini.
 
Back
Top Bottom