Hii Horoya imeingiaje Makundi ya Cafcl ? Mbona ni timu hovyo sana

mlambaji asali

Senior Member
Joined
Jan 30, 2023
Posts
150
Reaction score
505
Hawa wapinzani wa Simba kutokea nchini Guinea Horoya Athletic club ni wabovu sana aisee, Hawawezi hata kupasiana pasi tatu, hawawezi hata kufungua vyumba, wazito hakuna mfano, Yaani utafikiri ni timu ya daraja la nne.

Simba akishindwa kuchukua point 6 Kwa Hawa vibonde itabidi wajilaumu wenyewe
 
Hii ni timu au wahuni wa mtaani? Raja Casablanca atapiga goli 20 Hawa vibaka
 
Na mimi nimeona nikadhani labda mimi ndio sielewi mpira, hawa Horoya hapana aisee ni timu mbovu basi tu wamekutana na wabovu zaidi yao wakabahatisha kigoli kimoja icho lakini naona kabisa Raja casablanca watatembeza sana vichapo kwenye hili kundi
 
Makolo ni makolo tu, tulitegemea hata goli nne,lakini wao ndo wametobolewa
 
Haya washawaweka teyari na uzito walionao
 
Na wao wanawashangaa na ubovu wao wote ila wamewatoboa
 
raja ni wakawaida tu niliwaona jana, alafu hawa raja walipasuka 2-1 pale guinea mwaka jana nahawahawa horoya
Wanajua basi vichwa maji hao kazi yao ni umbea tu.

Kesho watapasuka nyingi na watasingizia wamepangwa kundi gumu
 
Ni kweli mkuu.
Horoya ni kama Namungo tu.
Simba kafungwa sababu ya ugeni tu, ila me nimefurahi kuzimwa ngebe zao.
 
Hawa ni mabingwa mara 8 mfululizo wa Guinea na kwa hapa Africa Guinea nawaweka level moja na Senegal, Ghana na Cameroon kwenye viwango.

Game ya leo kila mmoja alikuwa anamuogopa mwenzake kwa hiyo wakawa wanacheza kwa tahadhari, hii ni ligi ya wanaume miamba wa Africa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…