Hii ikoje wadau? Mtu ana gari no A anabadili na kupata D?

Hii ikoje wadau? Mtu ana gari no A anabadili na kupata D?

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,390
Hakika hii imenistua kidogo au ni ushamba wangu?. Jamaa yangu alikuwa na gari 'chakavu' namba A sasa sijui kafanyaje kaende TRA eti kafanya mbinu na kubadilishiwa na kupewa namba D kisha amelipiga rangi sasa liko sokonoi 'jipya' kabisa.

Hii ikoje? naomba mwenye uelewa
 
Gari imekuwa brand new
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mkuu sidhani kama inawezekana. Kwenye kadi ya gari inaandikishwa Chassis number na Engine number. Sasa haitawezekana kabisa hivyo vitu viandikwe sehemu mbili.

Hakika.Asilimia 100 ni gari ya rafiki yangu.siongelei hadithi hapa.mimi nilidhani haya yangefanyika katika uongozi uliopita kumbe sasa .
 
Mkuu sidhani kama inawezekana. Kwenye kadi ya gari inaandikishwa Chassis number na Engine number. Sasa haitawezekana kabisa hivyo vitu viandikwe sehemu mbili.
Kitaalamu na kisheria haiwezekani lakini usisahau TZ mgonjwa wa kichwa anafanyiwa operation ya mguu mkuu!
 
Hakika.Asilimia 100 ni gari ya rafiki yangu.siongelei hadithi hapa.mimi nilidhani haya yangefanyika katika uongozi uliopita kumbe sasa .
Ungeweka wazi, kwa kutanabaisha namba ya awali na namba ya sasa, ingesaidia sana kuelewa ukweli ukoje? Vinginevyo kuwa msamaria mwema kwa kupeleka taarifa TRA ili waweze kufatilia.
 
Taja namba ya gari kusaidia watu wasiingie mkenge...

Inamaanisha ni muhimu kucheki na zile namba zingine kwenye magari yenyewe ikiwa mtu anataka kununua.
 
inawezekana kisheria.. unatakiwa kua na vidhibitisho vya kufanya.. de-registration, unafanya hivyo de registration kwa gari ambalo unajua hutalitumia muda mrefu.... ili road license Penalty isiendelee kulimbikiza.... then ukiwa tayari kuanza kulitumia unalifanyia registration upya, taratibu zote hizi tunategemea zichukue miaka.., kama zimefanyika ndani ya mwezi.. basi hela imefanya kazi yake apo
 
Hakika hii imenistua kidogo au ni ushamba wangu?. Jamaa yangu alikuwa na gari 'chakavu' namba A sasa sijui kafanyaje kaende TRA eti kafanya mbinu na kubadilishiwa na kupewa namba D kisha amelipiga rangi sasa liko sokonoi 'jipya' kabisa.

Hii ikoje? naomba mwenye uelewa
Hiyo kadi ya gari no D sio ya kutoka Tra, ni kadi za kutengeneza mtaani, ukiweza kutengeza kadi ya gari ya kugushi kutengeneza plate number mpya number D hushindwi, hilo ni bomu litalipuka mtu akienda kurenew road licence
 
Hta hko tra kna bnadam so kila kitu knawezkana, tahadhari: kwa wanaoshobokea kununua gar kwa mtu et sababu kaambiw namba D, kwan namba D ndo uzima wa gari
Wewe ni Kinehe Magesa 😉😉🙁🙁🙁
 
Ungeweka wazi, kwa kutanabaisha namba ya awali na namba ya sasa, ingesaidia sana kuelewa ukweli ukoje? Vinginevyo kuwa msamaria mwema kwa kupeleka taarifa TRA ili waweze kufatilia.
Si anasema hiyo namba imepatikana huko huko TRA?
 
Back
Top Bottom