Hii ikoje wadau? Mtu ana gari no A anabadili na kupata D?

Hii ikoje wadau? Mtu ana gari no A anabadili na kupata D?

Utatafutwa mkuu ili ulionyeshe hilo gari lifuatiliwe, usije ukasumbua tu vyombo vya dola maana itakuhusu
 
uko tayari kutoa ushahidi
Mkuu badilisha hilo jina lako la BRN kwanza, maan mkulu ameshaipiga chini ameona haina tija ilikuwa kupeana ulaji tu na wale waliokuwa wameajiriwa pale magogoni sijui PDB wameshafukuliziwa mbali hawana chao, limebaki jina mtaan tu
 
Kama ilikuwa ni namba A na ilikuwa na namba za usajili za biashara yani nyeupe, ukibadili usajili kwenda kwenye namba za rangi ya Njano utapewa no D unaweza kana kwa njia hii
Hili ndio jibu, thanks
 
mbona unauliza swali ambalo jibu unalijua.
money talk,,,,,
 
Mkuu badilisha hilo jina lako la BRN kwanza, maan mkulu ameshaipiga chini ameona haina tija ilikuwa kupeana ulaji tu na wale waliokuwa wameajiriwa pale magogoni sijui PDB wameshafukuliziwa mbali hawana chao, limebaki jina mtaan tu
Nashukuru kwa taarifa Mkuu
 
Hii michezo inafanyika sanaaa, mfano unakuta gari Labda T300EAC ina daiwa deni kubwa TRA unachonga na watu wa TRA wanakupa namba mpya mzigo unakuw T300DGW kwa raha zako...hapo unakuwa ume escape kodi. Magufuli anakazi sanaaa
Kwa mfumo wa TRA,hakuna kitu kama hicho.
 
View attachment 369132
Inawezekana kabisa kubadili namba ya gari kisheria. Kwa mfano unaponunua gari kwa mtu na kuibadili umiliki unaweza pia kuomba kuibadili namba na rangi pia. TRA wanachofanya wanaiondoa ile namba na kumbukumbu zake zote za awali na kuingiza kumbukumbu mpya kwenye DATABASE yao. Unapokwenda kulipia Road license unakwenda na kadi mpya ile ya zamani haipo tena hewani. Ila inabidi ulipie gharama ya kubadili namba yaani unafanya usajiri upya na pia kama unataka kubadili rangi pia unalipa.
Kwa nini hamshangai watu wanatoa namba za magari na kuweka majina yao kwenye plate namba? Ni kulipa tu acheni kuwazushia TRA. Kama pikipiki zilibadilishwa namba za awali na kupewa mpya iweje gari ishindikane kubadilishwa namba kisheria?
Uko sahihi mkuu
 
Mkuu sidhani kama inawezekana. Kwenye kadi ya gari inaandikishwa Chassis number na Engine number. Sasa haitawezekana kabisa hivyo vitu viandikwe sehemu mbili.
Nami naungana nawe, Si rahisi sana kuchakachuka chassis number na kuisaji gari upya kwa sababu gari zote zinazosajiliwa kwa matumizi nchini humu zimeingizwa kwenye kompyuta za TRA na zinajulikana. Hilo suala la kubadili namba linawezekana tu iwapo gari ilikuwa na namba nyingine mfano DFP, PT, CD, ST... nk, kisha mtu akanunua kutoka taasisi husika na kubadili umiliki kuwa wa kiraia.
 
Back
Top Bottom