Hii ikoje wadau? Mtu ana gari no A anabadili na kupata D?

Utatafutwa mkuu ili ulionyeshe hilo gari lifuatiliwe, usije ukasumbua tu vyombo vya dola maana itakuhusu
 
uko tayari kutoa ushahidi
Mkuu badilisha hilo jina lako la BRN kwanza, maan mkulu ameshaipiga chini ameona haina tija ilikuwa kupeana ulaji tu na wale waliokuwa wameajiriwa pale magogoni sijui PDB wameshafukuliziwa mbali hawana chao, limebaki jina mtaan tu
 
Kama ilikuwa ni namba A na ilikuwa na namba za usajili za biashara yani nyeupe, ukibadili usajili kwenda kwenye namba za rangi ya Njano utapewa no D unaweza kana kwa njia hii
Hili ndio jibu, thanks
 
mbona unauliza swali ambalo jibu unalijua.
money talk,,,,,
 
Mkuu badilisha hilo jina lako la BRN kwanza, maan mkulu ameshaipiga chini ameona haina tija ilikuwa kupeana ulaji tu na wale waliokuwa wameajiriwa pale magogoni sijui PDB wameshafukuliziwa mbali hawana chao, limebaki jina mtaan tu
Nashukuru kwa taarifa Mkuu
 
Hii michezo inafanyika sanaaa, mfano unakuta gari Labda T300EAC ina daiwa deni kubwa TRA unachonga na watu wa TRA wanakupa namba mpya mzigo unakuw T300DGW kwa raha zako...hapo unakuwa ume escape kodi. Magufuli anakazi sanaaa
Kwa mfumo wa TRA,hakuna kitu kama hicho.
 
Uko sahihi mkuu
 
Mkuu sidhani kama inawezekana. Kwenye kadi ya gari inaandikishwa Chassis number na Engine number. Sasa haitawezekana kabisa hivyo vitu viandikwe sehemu mbili.
Nami naungana nawe, Si rahisi sana kuchakachuka chassis number na kuisaji gari upya kwa sababu gari zote zinazosajiliwa kwa matumizi nchini humu zimeingizwa kwenye kompyuta za TRA na zinajulikana. Hilo suala la kubadili namba linawezekana tu iwapo gari ilikuwa na namba nyingine mfano DFP, PT, CD, ST... nk, kisha mtu akanunua kutoka taasisi husika na kubadili umiliki kuwa wa kiraia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…