Eti
Rabbon wewe unasemaje? Dalili ya nini hiyo? 😆
Hiyo ni dhoruba/ tornado, ni kimbunga Cha baharini.
Na upepo unatokana na neno Pepo. Wapo Malaika wanaohusika kuendesha majira na Pepo kuu nne duniani.
Wapo pia miungu wafanyao uharibifu kutumia Pepo hizo hizo maana wameruhusiwa Kwa kiwango Fulani japo Wana limits.
Twende na huku.
(Ufunuo wa Yohana 7:1-4)
1: Baada ya hayo nikaona Malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia PEPO NNE ZA NCHI , upepo usivume juu ya nchi, Wala juu ya bahari Wala juu ya mti wowote.
2: Nikaona Malaika mwingine, akipanda Kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai, akawapigia kelele Kwa sauti kuu wale Malaika wanne waliopewa kuidhuru Nchi na bahari,
3: Akisema, msiidhuru Nchi wala bahari Wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya VIPAJI VYA NYUSO ZAO.
......END.....
Pia ujue, mvua ya mawe theluji na tufani ni silaha ambazo Mungu huzitumia kuwaokoa awapendao na kuwaangamiza maadui zake.
(Ayubu 38:22-23)
22: Je ! Umeziingia ghala za theluji, au umeziona ghala za mvua ya mawe,
23: Nilizoziweka akiba Kwa wakati wa misiba,
Kwa siku ya mapigano, Kwa siku ya mapigano na vita?