Hii inasababishwa na woga au mazoea?

Hii inasababishwa na woga au mazoea?

officialBossmtoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2019
Posts
370
Reaction score
1,189
Kwanza kabisa naomba kueleza moja kwa moja kwamba sina nia ya kuzusha mabishano, napenda mjadala huu uwe positive sababu ni kitu ambacho nimekishuhudia live.

Nikiwa kwenye bajaji ya kutoka Mbezi kwenda Mwenge tulikua abiria wanne na dereva. Kiti pembeni ya dereva alikua amekaa Binti ambae alikuja na abiria waliokuja kukaa nyuma. Hii inaonekana ilikua familia moja. Baba alikua amekula Kanzu safi na Kofia (Barakashia) na Mama amejisitiri vizuri kichwani mpaka miguuni. Mimi pekee nikiwa nimekaa ndani kabisa ubavuni na kipensi changu.

Katika kupanda daraja la Mfugale pale juu Bajaji ikachomoka gear. Mnaopanda bajaji mnajua kuna mlio wa resi unatokea basi pale ndo niliposhangazwa

BABA, Alisema kwanguvu bila woga YESU WANGU

BINTI, Pia nae vile vile alisema JESUS

MAMA, Kwa upole kabisa peke yake ndo alisema MTUME ROHO YANGU.

HII HALI YA KUKIMBILIA KULITAJA JINA LA YESU, LINALETWA NA WOGA AU NI MAZOEA?

Tujadili.
 
Yesuuuuu
Matendo ya Mitume 4:12
[12]Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Neither is there salvation in any other: for there is none other name under heaven given among men, whereby we must be saved.
 
Una audio au kavideo kuthibitisha! Hata Shigongo nae alikua anaishi kwa hizi stories
 
Yesuuuuu
Matendo ya Mitume 4:12
[12]Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Neither is there salvation in any other: for there is none other name under heaven given among men, whereby we must be saved.
Ni mazoea tu na hii hutokana na mazingira
 
Kwanza kabisa naomba kueleza moja kwa moja kwamba sina nia ya kuzusha mabishano, napenda mjadala huu uwe positive sababu ni kitu ambacho nimekishuhudia live.

Nikiwa kwenye bajaji ya kutoka Mbezi kwenda Mwenge tulikua abiria wanne na dereva. Kiti pembeni ya dereva alikua amekaa Binti ambae alikuja na abiria waliokuja kukaa nyuma. Hii inaonekana ilikua familia moja. Baba alikua amekula Kanzu safi na Kofia (Barakashia) na Mama amejisitiri vizuri kichwani mpaka miguuni. Mimi pekee nikiwa nimekaa ndani kabisa ubavuni na kipensi changu.

Katika kupanda daraja la Mfugale pale juu Bajaji ikachomoka gear. Mnaopanda bajaji mnajua kuna mlio wa resi unatokea basi pale ndo niliposhangazwa

BABA, Alisema kwanguvu bila woga YESU WANGU

BINTI, Pia nae vile vile alisema JESUS

MAMA, Kwa upole kabisa peke yake ndo alisema MTUME ROHO YANGU.

HII HALI YA KUKIMBILIA KULITAJA JINA LA YESU, LINALETWA NA WOGA AU NI MAZOEA?

Tujadili.
Mazoea au inawezekana ao watu wameaamia dini ya uislamu ndani ya mda si mrefu sidhan kama u
kuna muislam ambae yupo ndan ya dini kwa mda mrefu atasema Yesu au jesus
 
Mbezi to Mwenge via Mfugale.
Hii route siielewi au mimi sio mtoto wa mjini.
 
Back
Top Bottom