officialBossmtoto
JF-Expert Member
- Jul 1, 2019
- 370
- 1,189
Kwanza kabisa naomba kueleza moja kwa moja kwamba sina nia ya kuzusha mabishano, napenda mjadala huu uwe positive sababu ni kitu ambacho nimekishuhudia live.
Nikiwa kwenye bajaji ya kutoka Mbezi kwenda Mwenge tulikua abiria wanne na dereva. Kiti pembeni ya dereva alikua amekaa Binti ambae alikuja na abiria waliokuja kukaa nyuma. Hii inaonekana ilikua familia moja. Baba alikua amekula Kanzu safi na Kofia (Barakashia) na Mama amejisitiri vizuri kichwani mpaka miguuni. Mimi pekee nikiwa nimekaa ndani kabisa ubavuni na kipensi changu.
Katika kupanda daraja la Mfugale pale juu Bajaji ikachomoka gear. Mnaopanda bajaji mnajua kuna mlio wa resi unatokea basi pale ndo niliposhangazwa
BABA, Alisema kwanguvu bila woga YESU WANGU
BINTI, Pia nae vile vile alisema JESUS
MAMA, Kwa upole kabisa peke yake ndo alisema MTUME ROHO YANGU.
HII HALI YA KUKIMBILIA KULITAJA JINA LA YESU, LINALETWA NA WOGA AU NI MAZOEA?
Tujadili.