Muda wa masomo wa mwanachuo pamoja na chuo husika ndivyo vinavyoamua upatikanaji wa muda wa ziada kwaajili ya shughuli zingine. Kama ni mwanachuo wa 'full-time', mara nyingi muda wa ziada huwa ni hafifu ukilinganisha na mwanachuo wa 'part-time'.
Hata hivyo, si vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya 'part-time'. Hapa nazungumzia vyuo vikuu ambavyo kwa kiasi kikubwa huwa vinatoa mafunzo ya 'full-time' pekee. Kusoma kozi nyingine nje ya chuo inawezekana kwa uzuri zaidi kwa vyuo vinavyotoa mafunzo ya 'part-time'.