Hii kamatakamata ya Waandishi wa Habari na ukimya wa Polisi, ni hatari kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari

Hii kamatakamata ya Waandishi wa Habari na ukimya wa Polisi, ni hatari kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Nikiwa kwenye TV yangu nimefanikiwa kupata nafasi ya kumsikiliza Mkuu wa Nchi Rais Samia Suluhu Hassan kwa mara nyingine akisisitiza Uhuru wa Vyombo vya Habari, hii ilikuwa kwenye lile Kongamano la Wanahabari, Juni 18, 2024.

Alivyokamatwa Mwandishi wa kwanza katika sakata hilo ~ Mwandishi aliyeandika tuhuma za RC Simiyu adaiwa kukamatwa na Polisi

Kauli hiyo siyo mara ya kwanza kwa Rais kuitoa hadharani, mara kadhaa ameshazungumza hivyo na kweli ameonesha kwa vitendo kuwa suala la kukosolewa kwake siyo ishu kubwa, ana ngozi ngumu, lakini upande wa pili kinachoendelea kwa Waandishi wa Habari kule Mwanza na Mikoa ya Kanda ya Ziwa hakina afya kwenye tasnia ya Habari.

Hakuna Mtu aliye juu ya Sheria lakini Polisi wanatakiwa kuweka wazi tuhuma, mchakato wa dhamana au kuwafikisha Mahakamani wahusika kwa kuwa ni haki yao Kisheria.

Waandishi waliokamatwa mpaka sasa ni Dinna Maningo wa Mara, Samweli Mwanga na Costantine Mathias (wote wa Simiyu), tuhuma zinazotajwa kuwa ni kuvujisha ile ripoti ya Polisi kuhusu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda kuhusishwa na tukio la ulawiti.

“Kama haya yanatokea kwa Wanahabari wenye nafasi ya kupaza sauti, vipi kuhusu raia w kawaida ambao hatuna nafasi hiyo au ni njia ya kuwatisha Wanahabari? Je, ni mpango wa kuminya Uhuru wa Habari?

Dinna Maningo, Samweli Mwanga na Costantine Mathias wanatakiwa kufikishwa Mahakamani ili haki itendeke na siyo kuwakalisha kwenye Kituo cha Polisi na kisha kuwa kimya.

Ukimya unazidisha taharuki tu ambazo inawezekana wangeweza kumaliza jambo hili kwa mchakato sahihi wa kutoa taarifa ili Jamii ijue, kama ni suala la upelelezi nalo waweke wazi.

Kamanda wa Polisi wa Mwanza, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Waziri wa Habari na Waziri wa Mambo ya Ndani wawajibike kuondoa taharuki hiyo ili isionekane Polisi wanaenda kinyume na msisitizo wa Rais Samia ambaye amekuwa akisisitiza Uhuru wa Vyombo vya Habari chini ya utawala wake upo.


~ THRDC: Mwandishi aliyekamatwa akidaiwa kutumia nyaraka za siri bado hajapewa dhamana
~ Simiyu: Mwandishi akamatwa na Polisi
 
Back
Top Bottom