The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 2,471
- 3,768
Yaani hii kampeni ya nishati safi ni kampeni hewa ambapo hakuna uhusiano kati ya kelele zinazopigwa na hali halisi.
Siioni nia ya serikali kusaidia wananchi zaidi ya hadithi na porojo na propaganda zinazopigwa kwenye vyombo vya habari.
Bei ya gas inapanda kila kukicha wakati viongozi wako bize kugawa vimitungi.
Sasa unagawa mitungi ilihali bei ya ges inapanda kila siku?
Badala ya kutumia mamilioni ya pesa kufanya promo ya jambo hili hayo mapesa yalitakiwa kupelekwa kushusha bei ya ges.
Bei ya gas ikishuka hutahitaji kumtangazia Wala kumuekimisha mtu yeyote kuhusu nishati gani atumie.