Hii kauli inamaanisha nini wadau?

Hahaha
Fungua ubongo huo ng'amua mambo hiyo case ndogo sana.
Asante. Ndio maana nimeleta humu kwenye mawazo muyatoe. Msije sikia mtu kafanya maamuzi magumu mkaishia kulaumu shetani .
 
Hata mimi huo ujinga wa mtu alitoa tung'ombe tuwili ammiliki mwanangu akiwa hai na akiwa amekufa siuungi mkono.

Mama aliyezaa kwa uchungu eti hawezi kuamua mwanae azikwe wapi ila hayo mamlaka kanapewa kahuni fulani tu eti kwasababu kametoa tung'ombe tutatu.

Nimke wako akiwa hai, akifa akazikwe kwao ili angalau watoto wako wakienda kutembelea kabuli la mama yao wanapata fursa ya kujuana na ndugu zao upande wa mama.
 
Na haujasema chanzo cha yeye kusema hivyo, watu wanaopendana na kuishi kwa amani katika ndoa zao hawawezi kutoleana maneno kama hayo, ila navojua kuna hasira anayo iliyomjengea chuki ndani ya moyo wake hatamani hata siku akifa umzike wewe, ila ndugu zake akiwemo baba yake
 
Hata kama ni hasira ndio atoe maneno ya hivyo wakati Mimi ni mtu ninayeingilika kimazungumzo vizuri tu. Namhudumia vizuri.
 
Usipate shida, ukikaa nae kwa kutumia mpe peni na karatasi mwambia aandike yale aliyoyasema kwa herufi kubwa sana na aandike pia jina la baba yake na mawasiliano yake. Kama atakubali kuyaandika basi chukua gundi yabandike chumbani kwenu akiuliza mwambie kichwa changu kina mambo mengi nisije nikasahau ukifa
 
Unaumizwa kichwa na kauli ya maiti mtarajiwa. Kwani wewe uli plan kumzikia wapi?
 
Kuhusu kifo chake, Huna haki.. hiyo kazi ya ukoo wake..
 
"Ndoa si kwa ajili yako ni kwa ajili ya watoto"

"Ndoa si pete zinazonga mikono, ndoa ni upendo unabakia baada ya kuchoka kingono"

"Ndoa ni kukumbatia kaa la Moto"

"Ndoa ni Jua Kali"

"Ndoa ni joto"

"Ndoa si drama mbele ya watu nyomi, ndoa ya kweli huanzia Moyoni"

"Ndoa ni fumbo"

Dizasta vina: Ndoano๐ŸŽถ
 
Wakati mwingine unakua mbabe kidogo na ujiweke kama baba.Wanawake huwa na maneno mengi sana wakipewa muda waongee watakacho.Hawana kikomo wala kiwango kwenye kuongea.
 
Ndoa ni ngumu jamani ๐ŸŽต

Au mpaka mume alete ukimwi nyumbani ๐ŸŽต
 
A

Mara nyingi wanawake ambao walikosa mapenzi ya baba, huwa wanakuja kuwa wasumbufu sana kwa waume zao. Tatizo nikuwa anatamani wewe uwe kama baba yake na pia uplay part ya mumewe pia, ambayo inataka mwanaume strong kitabia na kiuchumi. Sasa kama umelega lega hapo ujue ni dharau ya hali ya juu. Pambana sana mkuu. Ndio maana wazee wetu walishauri tuoe kwenye familia nzuri, ilikuwa ni katika kuangalia hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ