Hii kauli inamaanisha nini wadau?

Hii kauli inamaanisha nini wadau?

Hata kama ni hasira ndio atoe maneno ya hivyo wakati Mimi ni mtu ninayeingilika kimazungumzo vizuri tu. Namhudumia vizuri.
Achana na huduma, mwanamke anapoamua kuishi na wewe hafuati huduma ila PENZI.. makwazo yakizidi yanaumiza yanaeka chuki moyoni, ukute yapo mambo anayavumilia yanajirudia kila siku hadi yanamjengea chuki mbaya sana juu yako anajikuta anaishi na wewe sababu tu "jamii itanionaje nikiachika"
 
Mwanandani wangu wa kike amekuwa na tabia kuvutia mambo kwao mathalani kuwafundisha watoto tamaduni za kwao ikiwemo lugha na kusifia mambo mengi ya kwao. (kabila lake).

Sasa Jana ghafla akaanza kumuongelea baba yake mzazi kiufupi siye aliyemlea alimzaa tu wakalea wengine hata MAHARI hakupokea yeye Wala kwenye harusi hakuja japo alikuwepo na alikuwa ni mwenye afya tu.

Mwandani akatamka NENO hili na kuliwekea msisitizo ambao sikumjibu lakini limenikaa kichwani nikaona nishirikishe jukwaa ambalo najua Kuna wenye msaada na hekima na wapumbavu pia. Kuwa siku "akitangulia mbele ya haki kabla ya baba yake mzazi, baba yake ndio atoe maamuzi ya yeye kwenda kuzikwa akasisitiza tena kuwa ikiwa maneno yake ie. mke hayatatekelezwa basi nitajilaumu sana maishani ni kana kwamba nitapata matatizo" kwa kwenda kinyume na matakwa ya marehemu.

Sasa wadau naombeni ushauri hapa Ina maana mimi Sina maamuzi juu yake pamoja na kumlisha na kumtunza kote?. Au ni mtunzaji akiwa hai akifa Sina langu?. Vipi Mimi nikitangulia atawapoteza wanangu wasijue kabisa asili ya baba Yao Wala shangazi, baba wakubwa na wadogo upande wangu?. Anamaanisha Nini?. Au INAMAANISHA Nini hii?.

Naombeni mawazo wadau.
Huyo mkeo atakuwa mnyakyusa ! Hili kabila Lina umimi sana,
 
Lipotezee,wanawake ni kama watoto wanaongeaga vitu vingi vingi sana,vingine hata havina maana visikuumize kichwa

Kama umemtolea mahari,wew ndo utaamua pa kuzikwa yeye
 
  • Thanks
Reactions: J C
Si umuache tu mkuu... Ina maana ubongo wako umeganda kias gan kujua n hakufai,.. Kuna mama mmoja wa rafiki yangu tu aliwai niambia kuzaa na mtu si lazima kuishi nae
 
Mwanandani wangu wa kike amekuwa na tabia kuvutia mambo kwao mathalani kuwafundisha watoto tamaduni za kwao ikiwemo lugha na kusifia mambo mengi ya kwao. (kabila lake).

Sasa Jana ghafla akaanza kumuongelea baba yake mzazi kiufupi siye aliyemlea alimzaa tu wakalea wengine hata MAHARI hakupokea yeye Wala kwenye harusi hakuja japo alikuwepo na alikuwa ni mwenye afya tu.

Mwandani akatamka NENO hili na kuliwekea msisitizo ambao sikumjibu lakini limenikaa kichwani nikaona nishirikishe jukwaa ambalo najua Kuna wenye msaada na hekima na wapumbavu pia. Kuwa siku "akitangulia mbele ya haki kabla ya baba yake mzazi, baba yake ndio atoe maamuzi ya yeye kwenda kuzikwa akasisitiza tena kuwa ikiwa maneno yake ie. mke hayatatekelezwa basi nitajilaumu sana maishani ni kana kwamba nitapata matatizo" kwa kwenda kinyume na matakwa ya marehemu.

Sasa wadau naombeni ushauri hapa Ina maana mimi Sina maamuzi juu yake pamoja na kumlisha na kumtunza kote?. Au ni mtunzaji akiwa hai akifa Sina langu?. Vipi Mimi nikitangulia atawapoteza wanangu wasijue kabisa asili ya baba Yao Wala shangazi, baba wakubwa na wadogo upande wangu?. Anamaanisha Nini?. Au INAMAANISHA Nini hii?.

Naombeni mawazo wadau.
Wewe siyo mumewe. Anakuona kama hawara tu, pengine hakupenda aolewe na wewe.

Muhimu: Fanya kama alivyofanya Hakimi, yule mcheza mpira. Utakuja kunishukuru hata kabla huu mwaka haujaisha
 
  • Thanks
Reactions: J C
Wewe siyo mumewe. Anakuona kama hawara tu, pengine hakupenda aolewe na wewe.

Muhimu: Fanya kama alivyofanya Hakimi, yule mcheza mpira. Utakuja kunishukuru hata kabla huu mwaka haujaisha
Asante kwa ushauri. Huyo Hakimi alifanyaje?. :
 
Back
Top Bottom