Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Ninajiuliza, kama mwanzo kodi hizi zilikua zinalipwa na wamiliki wa majengo, imekuaje mzigo huu utupiwe kwa wapangaji? Hii ni haki siyo uonevu?
Kwanini nisifikiri kuwa viongozi wetu huko juu ndio wengi wao wanamiliki majumba mengi kama miradi yao wanataka kukwepesha mzigo huu kwao? Kwanini umrundikie mzigo mnyonge huyu huyu ambaye mfumoko wa bei tu umemwandama alichilia mbali tozo zingine?
Kuna kila sababu ya kulifuatilia vizuri hili jambo kujua ni kwanini serikali imeamua kuwabebesha mzigo huu watu wa chini badala ya wamiliki, liko tatizo na nitabakia kuwaza kua ni mradi wa watu.
Magufuli asingeweza kuwabebesha mzigo huu raia wake, maumivu tunayaona baada ya yeye kuondoka. Yaani watu wanaamka tu na kumrundikia mzigo wa Tozo raia ambaye pesa ya kula tu bado shida.