mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Urusi ilialika watu au taasisi zinazohitaji kuwa waangalizi kwenye kura ya maoni iliyohusu majimbo manne ya ukraine kukubali kujiunga na Urusi au kubaki kwenye himaya ya Ukraine. Urusi ilikuwa na uhakika kabisa kuwa zoezi la kura litaendeshwa kwa uhuru na uwazi. Wapo watu wengi toka nchi za magharibi walijitokeza na taasisi binafsi pia, ila zimeshatishiwa zitachukuliwa hatuwa na mabeberu!
Kwa faida ya wale ambao hawakuwa wanafuatilia sakata hili toka 2014 ni kuwa: Hayo majimbo manne ya ukraine yaani mawili kule mashariki mwa ukraine yajulikanayo kama DONBASS na mawili kusini mwa ukraine sehemu kubwa ya watu wake (zaidi ya asilimia 90) ni warusi waishio ukraine na wana uraia wa ukraine. Kwa wao kuwa warusi hilo lilishakuwa balaa kwao toka hiyo 2014. Lugha ya Urusi hatimaye ilizuiwa kutumika kama moja ya lugha rasmi na haikuruhusiwa tena kutumika mashuleni kama hapo awali. Yale majimbo mawili ya DONBASS yaligomea utaratibu huo na kuamua kujitenga, hilo likazusha vita vikali na maelfu wakauawa kwenye vita hivyo. Yale majimbo ya kusini menyewe yalikosa ubavu wa kujitenga na ukraine maana hawakuwa na huo uwezo wa kuhimili vita kukabiliana na majeshi ya Ukraine japo walitamani pia kujitenga.
Ila kujitenga tu haikuwahakikishia usalama wa kudumu bali walitaka kujiunga na urusi ila urusi wakati huo haikuwa tayari kukubaliana na hilo. Warusi nchini ukraine wamekabiliana na manyanyaso sana kwa hiyo walivyopewa fursa ya kutoa maoni yao kama wanakubali kujiunga na urusi, kila mtu katika ulimwengu wa magharibi alijua kuwa lazima watakubali kwa kishindo kujiunga na urusi maana wamekuwa wakiomba hivyo tokea zamani. Ndiyo maana nchi za magharibi zilisema hazitakubali matokeo ya kura hiyo maana walijua hayo matokeo yatakuwa yapi. Kwa hiyo kuyauliza hayo majimbo manne kuhusu kujiunga na Urusi ni sawa na kumwuliza mbuzi aendelee kukaa mwituni au anataka arudi zizini kwa watu, jibu kila mtu analijua!
Ukraine imepoteza hayo majimbo manne jumla maana haiingii akilini kuwa kua siku wataishinda vita urusi na kuyateka tena!! Ila Marekani imefurahi maana imepata soko la kudumu la kuuza silaha zake maana huu mgogoro umekuwa wa kudumu maana Urusi itaendelea kudumu! Waliopata hasara kubwa ni Waukraine ambao wataendelea kumwaga damu yao kwa kutumikia matakwa ya marekani anayetaka soko la silaha zake! Marekani pia anaandaa mazingira ya soko la kudumu la kuuza silaha zake huko Taiwan!! Pia ana soko la kudumu huko Korea ya kusini na Japan!!
Wengine waliopata hasara ni Ulaya magharibi (EU). Marekani amewaharibia upatikanaji wa gesi na mafuta toka urusi kwa bei nafuu na watalazimika kununua gesi toka marekani kwa bei juu milele.