Hii kwangu imekuwa changamoto kubwa. Hata natamani kukimbia home

Hii kwangu imekuwa changamoto kubwa. Hata natamani kukimbia home

Mimi nimekaa na wadudu Hadi wamekuwa.part of me..Mende, gecko and the like..Mama hataki madawa yakuulia wadudu anasema sumu..

Nge nimeua sana, tandu and the like.. nyoka Mama alikua anaua tukishirikiana
Japo siku nyingi sijakutana na nyoka.. Alhamdulilah.

Wadudu hawanipi shida Sanaa labda kunguni
 
Mkuu ulimkimbiza duma wap, na huyo fisi wap? , Mbna kama kamba hii umetupiga, tatzo lako hujazoea hao wadudu na hyo ni Kwa sababu umezaliwa town na umekulia hapo town, mbwa huwaogopi c'se umekua ukiwaona unakutana nao unaona jins watu wanavyowatreat so uko aware nao, badlisha mtazamo wa fikra wachukulie Tu hao ni wadudu na jukumu lako ni kuwakabili na ukilegea wanakudhuru ...simple tuu , tofaut na hapo utaendelea kuwa muoga na hao wadudu wenyewe wapo Tu enzi na enzi na hawawez Isha , popote Tu wakiona fursa ya kuishi wanaishi... Kunguni na mbu ndo wadudu ambao sipatani nao kabisa hata kuwaona tuu ila hawaniogopeshi

Usitumie nguvu Sana kutuaminisha et huogopi hata Simba ila ukiona Mende unachora ...
labda aliwakimbiza huko Changanyikeni
 
Huku niliko kwangu kuna nyoka sana na kupambana nao ni jambo la kawaida, nilishawahi kung'atwa na kisa nikaleta humu.
Kuna majoka ya kila aina haipiti wiki lazima uwaone au uwaue wawili watatu na mpaka juzi saa moja usiku tumeua joka lenye unene wa tyre ya gari likitoka maeneo yangu na wenyeji wa huku wanaliita Bafe na kusifu kuwa ana sumu kali sana hivyo huua haraka sana.
Mazingira yeyote yanapokutokea usiogope bali jenga ujasiri! Mimi hadi hapa nilipo sasa hivi nimepumzika hapa ndani lakini najua kama sio chini ya kitanda basi nyuma ya makabati kuna nyoka, maana kila baada ya muda nakuta gamba nene jeusi lililo vuliwa na nyoka.
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mimi nimekaa na wadudu Hadi wamekuwa.part of me..Mende, gecko and the like..Mama hataki madawa yakuulia wadudu anasema sumu..

Nge nimeua sana, tandu and the like.. nyoka Mama alikua anaua tukishirikiana
Japo siku nyingi sijakutana na nyoka.. Alhamdulilah.

Wadudu hawanipi shida Sanaa labda kunguni

Mungu Ashukuriwe, mie mwenyewe nishaua nge na tandu sana... Kuna siku zamani huko nipo kama 14 yrs niliua 3 snakes in a day kwa time tofauti tofauti.... alipokuja kuonekana wa nne niliwambia mie huyo simgusi mana hawa watakuwa sio snakes wa kawaida coz walikuwa size moja rangi moja time tu walikuja tofauti [emoji83][emoji2]. Yaani kwetu ilikuwa akionekana mdudu naitwa mie ndio nlikua starring wao. Ajab saivi ndio nimekuwa mwoga mwoga yaani hata sipendi kuona wadudu wadudu
 
Nyoka wa kijani hangati kutokana na maumbile ya meno yake, hana meno kwa mbele, meno yake yameanzia katikati ya taya, hivyo kungata mpaka umkanyage na ahangaike kutoka
Nyoka wa kijani hawanaga madhara,unaweza lala nae ktandani,tuliwah ishi mahala walkuwa weng sana lakin hawakuwah kuleta madhara mwanzo tuliwauwa sana kwa sku tulkuwa tunaua watatu mpaka watano,jamaa mmoja akatueleza kuwa waacheni tu hawana shida mpaka Leo Mimi kama nyoka hayupo ndani hata kama ni wale weusi siwezi kumuua ni dhambi pale hajafanya kosa lolote why umuue
Wakuu hapa naona umeseleleka na mazoea.

Ni kweli Kuna nyoka wa kijani wasio na madhara (Green Grass Snakes, Green Rough Scale snakes na Green Snakes) Hawa unaweza hata kucheza nao lakini don't take a chance Kama huwezi kuwatambua nyoka kwa muonekano wao na sio rangi yao peke yake.

Kuna nyoka wa kijani wenye madhara Kama Boomslang na Green Mamba Hawa usijaribu kunyoosha mkono uwashike na uzuri au ubaya wao mbinu yao ni moja "Wait and see" kifupi patience ni silaha yao.

Green Mamba akikung'ata huna hata saa ya kuishi Kama utakosa msaada, sumu yake huathiri mfumo wa fahamu na moyo. Na kwa faida ya watu wa pwani Green Mamba wanapatikana Sana pwani ,Tanga, Dar es Salaam, Morogoro mtwara na Lindi.

Boomslang ni mpole na watu huzani hana madhara lakini katika nyoka wa kijani mwenye sumu Kali na yeye yumo akikuuma unaweza pitisha masaa bila kuona madhara na hapa wengi wamekufa pasipo kujua kwasababu ya kupuuzia. Sumu yake huathiri mfumo mzima wa damu.

Ukimsogelea Green Mamba Kama yupo Chini husimama hii ni ishara ya mapambano na Kama akiamua kukufukuza hufiki mbali.

Ukimsogelea Boomslang hutengeneza umbo "S" tayari kuattack yeye Hana tabia ya kufukuza. All in all kama huwezi kuwatambua chukua tahadhari, binafsi naweza kuwatambua but I never take a chance to belittle them.

Chizi Maarifa
Nyoka ni ngumu kupambana nao lakini unaweza ukachukua hatua chache wasifanye makazi yako kuwa makazi yao.

👉Mosi hakikisha ujenzi wa nyumba yako umezuia penyo kwa nyoka kuingia ndani ya nyumba hapa namaanisha milango na madirisha yawe well fitted
👉Hakikisha chemba za maji machafu zimefunikwa na mifuniko sawasawa bila kuacha nafasi
👉Fukuza au ondoa upatikanaji wa chakula Cha nyoka Kama vyura, mijusi,konokono,vinyonga,panya etc
👉Ondoa maficho ya nyoka Kama mashimo, nyufa, na pia nyoka hupenda kukaa kwenye sehemu zenye giza vivuli vizito na zenye unyevu
👉Fuga mifugo inayokula nyoka Kama Turkey (Bata mzinga) Nguruwe (Samahani Kama nimekukwaza kiimani) na Guinea Hens (Hawa nadhani ni Kanga)
👉Kuna harufu nyoka huwa hawapendi na moja ya harufu wasiyoipenda ni Moshi was Moto Kama mapira so you can smoke them out hili hufanyi kwa siku moja yawezakua wiki nzima Moshi haukati
👉Panda mimea inayofukuza nyoka Kama Michaichai kuanzia getini
👉 Landscaping, fyeka majani na epuka vichaka nyumbani
👉Chunguza fence yako kwa ndani na kwa nje Kama Kuna mashimo na nyufa ziba.

Mengine ni expensive Kama kuspray mafuta ya karafuu na mdalasini kwa wakati moja.

Salaam.
 
Dah pole mkuu ila mwanaume kuogopa wadudu kama mende na nyoka ni ajabu sana.

Njia nzuri ya kuzuia wadudu ni pamoja na kuhakikisha kuwa maeneo ni masafi ili kupunguza kuzaliana kwa wanyama kama panya wanaovutia nyoka, pia mazingira masafi yatapunguza wadudu kama mende na mbu hivyo hata hao mijusi watapungua.

Fumigation mara kwa mara itasaidia pia.
Nyoka huogopi wewe? Mimi naogopa hata picha yake.
 
Nyoka wa kijani hawanaga madhara,unaweza lala nae ktandani,tuliwah ishi mahala walkuwa weng sana lakin hawakuwah kuleta madhara mwanzo tuliwauwa sana kwa sku tulkuwa tunaua watatu mpaka watano,jamaa mmoja akatueleza kuwa waacheni tu hawana shida mpaka Leo Mimi kama nyoka hayupo ndani hata kama ni wale weusi siwezi kumuua ni dhambi pale hajafanya kosa lolote why umuue
Tooba..hilo eneo siwezi kukaa asilani
 
Mm sipendi mnyama paka....
Tena
Ile anakufuata na mkia wake anakugusa gusa sipendi mnyama anaitwa paka Wala huwa sipendi anisogelee...
Kuna siku nilikua nimekaa grossary na Rafiki zangu wawili wadada....
Tukawa tunakula nyama ya mbuzi ilikua jioni
Mapaka ya kibabe yakawa Yana zengea zengea nyau nyau mm nimepiga buyu....ile Sina hili Wala like paka mmoja akaja kunikwapua nyama mkononi
Nilishituka mpka wale wadada WALISHANGAA....
Binafsi nachukiaga paka Ila sio kwamba nawaogopa...
Sitamani hata kuguswa au kumshika huyo kiumbe...
 
Nashangaa had kahama twn wazee kuna kamtaa kanaitwa phantom kuna nyoka kilaa sku huku nyuma tunauwaa nmenusurika kukanyaga mara 2 nyoka kahama mjin
 
Huku niliko kwangu kuna nyoka sana na kupambana nao ni jambo la kawaida, nilishawahi kung'atwa na kisa nikaleta humu.
Kuna majoka ya kila aina haipiti wiki lazima uwaone au uwaue wawili watatu na mpaka juzi saa moja usiku tumeua joka lenye unene wa tyre ya gari likitoka maeneo yangu na wenyeji wa huku wanaliita Bafe na kusifu kuwa ana sumu kali sana hivyo huua haraka sana.
Mazingira yeyote yanapokutokea usiogope bali jenga ujasiri! Mimi hadi hapa nilipo sasa hivi nimepumzika hapa ndani lakini najua kama sio chini ya kitanda basi nyuma ya makabati kuna nyoka, maana kila baada ya muda nakuta gamba nene jeusi lililo vuliwa na nyoka.
Mzee baba unamoyo aisee, ningekuwa nishahama kitambo hapo. Dah, bafe nimwone na niendelee kukaa hapo, bafe yule hatari, ligi moja na cobra.
 
Kama umezungushia ukuta ni vzr.. chukua Oil chafu.. mwaga chini kuzunguka nyumba.

Pili Tumia Dawa kali ya Fumigation puliza miti na vichaka vyote.

Unaogopa mende... Hehe last week nilivyokuw MAPORINI nimelala na TANDU mweusi kitandani kilichonishtua ni zile sharubu zake alikuw ananigusa gusa maskioni.. nikawasha Taa nilizan ni mdudu tu wa Kawaida nikamkuta Tandu.. so ni vitu vya kawaida.. hapa kwenyewe nishaua KENGE.. mdg lkn alikuwa anasumbua sumbua nje.
Huyo kenge mbanike tu umle na ugali
 
Dah pole mkuu ila mwanaume kuogopa wadudu kama mende na nyoka ni ajabu sana.

Njia nzuri ya kuzuia wadudu ni pamoja na kuhakikisha kuwa maeneo ni masafi ili kupunguza kuzaliana kwa wanyama kama panya wanaovutia nyoka, pia mazingira masafi yatapunguza wadudu kama mende na mbu hivyo hata hao mijusi watapungua.

Fumigation mara kwa mara itasaidia pia.
Fumigation???.Naona mnaitaja sana lkn Sijui km mnafahamu maana yake?!!!!.
 
Ondoa mazingira ya wao kuwepo
 
Back
Top Bottom