Hii mimba jamani, mwenye uelewa..

Hii mimba jamani, mwenye uelewa..

Hivi mleta thread amesema mkewe anatokwa na damu zisizoeleweka au amesema alipata hedhi kwa siku nne baada ya hapo walipopima ndio akaonekana ana ujauzito. Kwani amekuambia damu zinaendelea kutoka? Usitufanye kana kwamba hatuji haya mambo. Unajifanya unajua kumbe bure kabisa

Kwahiyo damu zikiacha kutoka maana yake haiwezi kuwa ectopic?
 
Inawezekana vile vile hiyo bleeding ilikuwa PID

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwahiyo damu zikiacha kutoka maana yake haiwezi kuwa ectopic?
Damu za ectopic haziwezi kutoka kwa mfumo wa hedhi, huwa zinatoka kidogodogo na huwa nyingi pale mirija inapokuwa imepasuka.
 
Damu za ectopic haziwezi kutoka kwa mfumo wa hedhi, huwa zinatoka kidogodogo na huwa nyingi pale mirija inapokuwa imepasuka.

Sasa soma post yangu ya kwanza halafu soma tena ulichoandika hapa.

Mwanamke mwenye mimba hawezi kupata siku zake, ila anaweza kubleed. damu yake inakuwa ndogo kulikoo ya hedhi.

Akipata damu kama ya hedhi kwa siku nne, mimba HAIWEZI kuwepo.

Kipimo cha mkojo kinaweza kuwa positive hata kama mimba imetoka. Give it sometime akapime tena mkojo na ikiwezekana ultrasound.

Kipimo specific zadi ni concentration ya HCG kwenye damu, lakini nimewahi kuulizia kama kuna sehemu wanafanya Dar es Salaam sijapata jibu.

Ni muhimu aende hospitai ili afuatiiwe kwa sababu kuna risk ya ujauzito kuwa umetunga nje ya kifuko cha uzazi.

Kuhusu mirija kupasuka: kama unasoma kwenye google kuwa mwangalifu. Unajua mirija iko sehemu gani? Yaani mrija upasuke halafu damu zitoke ukeni? HAKUNA kitu kama hicho. Mrija ukipasuka damu inamwagika tumboni na ni emergency inayohitaji kufanyiwa operation haraka sana.

Swali la nyongeza: Je, kutokana na history iliyotolewa na mleta mada unaweza ku rule out ectopic?
 
Hivi mleta thread amesema mkewe anatokwa na damu zisizoeleweka au amesema alipata hedhi kwa siku nne baada ya hapo walipopima ndio akaonekana ana ujauzito. Kwani amekuambia damu zinaendelea kutoka? Usitufanye kana kwamba hatuji haya mambo. Unajifanya unajua kumbe bure kabisa

Mkuu nitonye,unamvunjia bure heshima yake mkuu ZeMarcopolo,kwani amekuwa msaada mkubwa kwetu hapa Jf doctor.
Hizo siasa zenu za u CCM na u CHADEMA mkalumbane jukwaa la siasa tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana vile vile hiyo bleeding ilikuwa PID

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Kwanini PID itoe damu nyingi kama za hedhi? Microbe gani anayeweza kusababisha PID ya namna hiyo?

Kitu gani kisababishe isimame baada ya siku nne?
 
Bwana Mundu tatizo sio Mimba. ishu ni mwanamke kushika mimba na bado akaingia ktk sku zake. this have been strange to me. siko hapa kulalamikia mimba. niko hapa kushere experience katika hili. Thanks.
This have? Kushare experience? Wewe una experience gani katika hilo? Tueleze. Kama ana mimba basi hiyo siyo yako.
 
Mkuu nitonye,unamvunjia bure heshima yake mkuu ZeMarcopolo,kwani amekuwa msaada mkubwa kwetu hapa Jf doctor.
Hizo siasa zenu za u CCM na u CHADEMA mkalumbane jukwaa la siasa tafadhali.
Tatizo liko pale anaposema kuwa huyo mama anaweza akawa na tatizo la ectopic. Damu ya ectopic ni tofauti na ile ya hedhi na huwa inatoka halafu inakata haipo kwenye mfumo wa hedhi. Labda kuna tatizo lingine. Then dalili za ectopic siyo kutokwa na damu pekee bali mwanamke anaweza
:kuhisi mabega kuuma
:kutapika na kuharisha
:kusikia maumivu wakati wa kukojoa
Halafu anasema kuna uwezekano mimba ikawa imetoka eti kisa mtu kapata hedhi. Na damu ya mimba iliyoharibika huwa na mabongemabonge
 
Last edited by a moderator:
Habarin jamvini... Naomba experience na utaalam wenu kuhusu hii mimba.

-Tarehe 21march,2013 nilikutana naye kimwili (bila kinga)
-Tarehe 10 April, 2013 akaingia bleed kama kawaida.
-Siku chache baada ya bleed kukata (ilimchukua siku 4 na ndo kawaida kwake) akaanza kuhisi dalili za ujauzito..nikamshauri akapime.
-Jana April 17 amepima na majibu yanaonyesha ni mjamzito.

katika experience yangu ya haya mambo hiki ni kitu kigeni kwangu.

NB: MHUSIKA NI MKE WANGU HALALI WA NDOA NA HII NI MIMBA YAKE YA KWANZA.

Hiyo blees ya tarehe 10 April ilikuwa kawaida kabisa na normal kama ya miezi mingine ya nyuma au it was just spotting??? yaani matone matone au siku moja kidogo tu? as tunaposema period lazima iwe normal
 
Tatizo liko pale anaposema kuwa huyo mama anaweza akawa na tatizo la ectopic. Damu ya ectopic ni tofauti na ile ya hedhi na huwa inatoka halafu inakata haipo kwenye mfumo wa hedhi. Labda kuna tatizo lingine. Then dalili za ectopic siyo kutokwa na damu pekee bali mwanamke anaweza
:kuhisi mabega kuuma
:kutapika na kuharisha
:kusikia maumivu wakati wa kukojoa
Halafu anasema kuna uwezekano mimba ikawa imetoka eti kisa mtu kapata hedhi. Na damu ya mimba iliyoharibika huwa na mabongemabonge

Je, unaweza kurule out ectopic pregnacy kwa kuangalia jinsi damu inavyotoka?

Hizo dalili za ectopic pregnancy sijui umetoa wapi, lakini just so that you know ectopic pregnancy au pregnancy of unknown localization ni topic kubwa na huwezi ku rule out kabla hujafanya vipimo maalum.

Kupata hedhi maana yake ni kwamba damu imetoka. Kama damu kutoka sio dalili ya mimba kutoka, sijui kuna dalili gani nyingine. Labda tusaidie kujua dalili ya mimba kutoka ni nini?
 
Sasa soma post yangu ya kwanza halafu soma tena ulichoandika hapa.

Kuhusu mirija kupasuka: kama unasoma kwenye google kuwa mwangalifu. Unajua mirija iko sehemu gani? Yaani mrija upasuke halafu damu zitoke ukeni? HAKUNA kitu kama hicho. Mrija ukipasuka damu inamwagika tumboni na ni emergency inayohitaji kufanyiwa operation haraka sana.

Swali la nyongeza: Je, kutokana na history iliyotolewa na mleta mada unaweza ku rule out ectopic?

jambo usililijua ni usiku wa giza... hii ya mirija kupasuka apart from ectopic pregnancy, mimba kutunga nje ya kizazi, kwenye mirija sijui inaweza sababishwa na nini... mkuu ZeMarcopolo kuna bush wengi sana aisee tuenelee tu kuelimisha pole pole ila wanakuwaga wabishi kweli
 
Last edited by a moderator:
Bwana Mundu tatizo sio Mimba. ishu ni mwanamke kushika mimba na bado akaingia ktk sku zake. this have been strange to me. siko hapa kulalamikia mimba. niko hapa kushere experience katika hili. Thanks.
inatokea mkuu.kitaalamu tunaita Arias -Stella reaction or phenomen.na huwa inatokea wakati yai lililorutubishwa linapandikizwa kwenye nyumba ya uzazi(implantation). sio wanawake wote wanaopata hali hii ila baadhi yao.na damu yake ni kidogo sana.Kama mlipima kwa kutumia planotest/UPT strips, false positive results inaweza kutokea, mfano inapotokea damu au cervical mucus imeingia kwenye mkojo.Pia abortions whether uterine abortion au tubal abortion au any early miscarriage yaweza kuonyesha positive results.Vuta muda halafu apime tena, au afanye pelvic scan(sonography) kuthibitisha kama kweli ni mjamzito.
 
Je, unaweza kurule out ectopic pregnacy kwa kuangalia jinsi damu inavyotoka?

Hizo dalili za ectopic pregnancy sijui umetoa wapi, lakini just so that you know ectopic pregnancy au pregnancy of unknown localization ni topic kubwa na huwezi ku rule out kabla hujafanya vipimo maalum.

Kupata hedhi maana yake ni kwamba damu imetoka. Kama damu kutoka sio dalili ya mimba kutoka, sijui kuna dalili gani nyingine. Labda tusaidie kujua dalili ya mimba kutoka ni nini?
Unaambiwa kaenda kupima na mimba kaikuta sasa tunabishania nini labda kama ana tatizo lingine. Kumbuka tunaongelea matokeo tuliyopatiwa na huyo mdau sio mabishano ya nani anajua nini. Then naomba unipe dalili za ectopic then aulizwe huyo kama ana dalili moja wapo.
 
Unajua nyinyi vijana wa bavicha ndio huwa mnasababisha watu wasiwe wanatumia ujuzi wao kutoa ushauri wa kitaalam.

Kuna watu wanatoa ushauri ambao kimsingi ulitakiwa kulipiwa, wanatoa bure tu. Halafu unatokea mtu kama wewe kuingiza siasa. Sasa hapa siasa imeingiaje?

Tatizo lako unadhani hili ni swala la udaku!
Ngoja nikujulishe basi ili next time ujifunze kuwa serious katika mambo serious. Hii habari iliyotolewa kwa kiasi kikubwa inaweza kumaanisha kuwa ujauzito uko nje ya kifuko cha uzazi. Kama ikiwa hivyo, ujauzito unaweza "kutoboa" mishipa ya damu na kusababisha damu nyingi kubwagika tumboni na kusababisha madhara makubwa ikiwemo kupoteza maisha.

Kwahiyo, habari hii sio ya kuifanyia mzaha. Ni jambo serious linalotakiwa kuchukuliwa kwa uzito unaostahili.

Tafadhali usirudie kuleta kejeli za siasa kwenye hili jukwaa.
nafikiri tuanze kutoa ushauri kwa ku-PM wahusika.
 
Unaambiwa kaenda kupima na mimba kaikuta sasa tunabishania nini labda kama ana tatizo lingine. Kumbuka tunaongelea matokeo tuliyopatiwa na huyo mdau sio mabishano ya nani anajua nini. Then naomba unipe dalili za ectopic then aulizwe huyo kama ana dalili moja wapo.

Umejiuliza alipima kwa kutumia method gani? What are limitations of that method.
 
jambo usililijua ni usiku wa giza... hii ya mirija kupasuka apart from ectopic pregnancy, mimba kutunga nje ya kizazi, kwenye mirija sijui inaweza sababishwa na nini... mkuu ZeMarcopolo kuna bush wengi sana aisee tuenelee tu kuelimisha pole pole ila wanakuwaga wabishi kweli

ZeMarcopolo ametoa sababu mbili za huyo mama kutokwa na hedhi, mosi huenda mimba ikawa imetoka pili anaweza akawa na ectopic kitu ambacho sio kweli. Mama mkwe hujambo lakini
 
Last edited by a moderator:
Umejiuliza alipima kwa kutumia method gani? What are limitations of that method.
Huwezi kucomplicate kiasi hicho hadi unasema eti umeulizia kipimo hata Dar es salaam hakuna. Mbona unakuwa mwongo wewe kwani utrasound hawezi kupimia?
 
Mweee.....pamoja na yote..... nitonye na ZeMarcopolo.....asanteni.......nimejifunza kitu kutoka kwenye sebene lenu.......
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom