Unajua nyinyi vijana wa bavicha ndio huwa mnasababisha watu wasiwe wanatumia ujuzi wao kutoa ushauri wa kitaalam.
Kuna watu wanatoa ushauri ambao kimsingi ulitakiwa kulipiwa, wanatoa bure tu. Halafu unatokea mtu kama wewe kuingiza siasa. Sasa hapa siasa imeingiaje?
Tatizo lako unadhani hili ni swala la udaku!
Ngoja nikujulishe basi ili next time ujifunze kuwa serious katika mambo serious. Hii habari iliyotolewa kwa kiasi kikubwa inaweza kumaanisha kuwa ujauzito uko nje ya kifuko cha uzazi. Kama ikiwa hivyo, ujauzito unaweza "kutoboa" mishipa ya damu na kusababisha damu nyingi kubwagika tumboni na kusababisha madhara makubwa ikiwemo kupoteza maisha.
Kwahiyo, habari hii sio ya kuifanyia mzaha. Ni jambo serious linalotakiwa kuchukuliwa kwa uzito unaostahili.
Tafadhali usirudie kuleta kejeli za siasa kwenye hili jukwaa.