Hii misemo ya kijamaa imepotelea wapi ndugu zangu?

Hii misemo ya kijamaa imepotelea wapi ndugu zangu?

Njaa na uchoyo vimetawala na kutamalaki miongoni mwa watanganyika.

Ukienda kwa ndugu hasa wa DAR roho zinawafurukuta wanahisi utawamalizia MAUGALI YAO.

MAUGALI yanafichwa uvunguni mpaka mida ya wanga ndo wanayatoa wanaanza kubugia fasta fasta kama wachawi.

Nyama zinafichwa kwenye SOKSI.

Huwa nashangaa mpaka mdomo unabaki wazi.

Cc: Lamomy cocastic Bolotoba Half american Mbaga Jr Extrovert Poor Brain secretarybird Monetary doctor
Huku mikoani, tumeambizana , ukienda kwa ndugu yako dar,..fahamu kuwa hapendi uguse chakula chake....hao watu wa dar ni watu wa aina ya kipekee sana, uchoyo wanasomea chuo na vyeti wanapewa..🚮🚮
 
Maisha ya zamani ilikuwa raha tupu:-​
  • ''Ingia bandani kamata kuku wawili tuchinje''​
  • ''Ingia shambani vunja mahindi tuje tuchome''​
  • ''Chemsha kahawa hapo jikoni ulete tunywe huku ukinihabarisha habari za huko nyumbani''​
  • ''Hadithi hii inatufundisha nini wajukuu zangu?''​
Nyakati hizi huwezi kupata hizi kauli.
Weee wa wapi? Mimi kwangu wageni wakija nawaambia "ebu tuhahirishe maongezi tuhudumie meza kuu". Hapo vyuku, misosi hatari! 😁😍😛
 
Back
Top Bottom