Hii Mitandao ya Jamii ina mambo!

Hii Mitandao ya Jamii ina mambo!

Wapo hao.
Tuliwahi kusimuliwa na jamaa mmoja tukiwa chuoni kuwa alikuwa anawasiliana na jamaa (mwanaume) kwa text sms, akawa hadi anatumiwa vocha! mara zote akiwa anapigiwa simu hapokei kwa visingizio kibao!
Tatizo ni tamaa, ujue hawa wanawake huwezi kuwamaliza hata ufanyeje,dawa ni kuridhika tu kwenye catchment area yako baaas!
 
Miezi 2 iliyopita rafiki yangu mmoja alinipa taarifa juu ya mahusiano na mdada mmoja aliyempata kwa njia ya Mtandao mmojawapo wa kijamii, uitwao face book. Kwa maelezo yake, amekuwa akiwasiliana na huyu dada pasipo kuonana naye kwa takriban mwaka na nusu sasa. Uhusiano wao ulikuwa mzuri mno kiasi hata cha kufikia kupeana emails, majina yao halisi na picha ambazo kimsingi zilionyesha uhalisia wa mawasiliano yao!

Kilichokuwa kikimsibu huyu jamaa ni kuwa dada huyo alikuwa akikataa kata kata kuonana na huyo kaka, ingawa maelezo ya kuchat ya kila siku through emails and yahoo messenger na SMS (alitoa namba ambayo ilikuwa blocked kwenye voice call) yalionyesha dada kumpenda kaka kupita maelezo.

Kaka amekuwa akijitahidi kutuma vocha na vijisenti kupitia MPesa kwa ajili ya matumizi kwa takriban mwaka sasa akiamini kuwa ipo siku dada huyo angemkubali maana kuna kipindi rafiki yake mwingine aliwahi kuoa kupitia face book.
Juzi kapokea sms kutoka kwa huyo dada, kuwa yeye ni mwanaume na siyo dada na aliamua kumlia pesa kwa kipindi chote hicho na anamshauri atafute mke badala ya kuendekeza online dating!

Swali: Hivi kweli kuna midume inayojifanya midada kwenye mtandao ya kijamii? Na kwanini wanafikia kufanya haya mambo? Na ni kweli dada huyo ni mwanaume au kamchoka tu huyo kaka na kumtumia msg hiyo kwa lengo la kumkatisha tamaa?

Wenu,
HP


Hahahhahahahhahaahhaahahaaaaaa.................duuhh, duniani kuna mambo.
 
Mjini shule!
Mwambie aendelee tu kumtumia hizo hela labda anaweza kumpata siku moja
amkameruni!


Hahahahhahahahahahahahaaaaaa..........Khaaaaa!
 
Internet dating niya kupeana faraja tu,nakupenda dear and al that kama ukiwa hauna mpenzi.au hujampata,lakini ndoa?..sijui.jaribuni
 
Back
Top Bottom