Hii nafasi ya Makamu wa Rais, mbona huwa tunaletewa watu wa ajabu sana?

Hii nafasi ya Makamu wa Rais, mbona huwa tunaletewa watu wa ajabu sana?

Hiyo ni nafasi ya kusubiria kiti kikuu kibaki wazi tu kabla ya muda uliopangwa jambo ambalo hutokea kwa nadra sana. Ukiangalia kiundani ni kupoteza pesa za umma tu kuwa na vyeo vya makamu wa rais na waziri mkuu kwa pamoja.
Niliwahi kufikiri cheo hicho kifutwe na kazi zake apewe Waziri mkuu au cheo cha Uwaziri mkuu kifutwe majukumu apewe Vice president kama Kenya .Sioni sababu ya kuwa na Makamu wa Rais kwa sasa NCHINI
 
KUsema ukweli japokuwa siwapendi ccm wote ila Nchimbi anaweza kutufanya tukaburudika mda wowote maana ameamua kuchagua haki kwanza
 
Tangu kuingia kwa vyama vingi vya siasa na kufanyika uchaguzi mwaka 1995, hatujawahi kuwa na makamu wa rais anayeeleweka.

Mkapa ndio alianza na alituletea kitu cha ajabu kabisa. Dr Omary Ally Juma. Jamaa alikuwa kituko aisee. Amekaakaa kwenye hiyo nafasi kama boya

Baada ya kifo cha dr Omary Ally Juma, mwaka 2001 mzee mkapa akatuletea Dr Ally Muhammed Shein. Huyu naye alikuwa urojo kabisa. Hapa jf alikuwa akitambulika kama ngariba. Kwa sababu alikuwa akitembea na mkasi. Kifupi alikuwa sio kiongozi alikuwa anatumwa kuwasha mwenge na kuuzima. Kukata utepe kwenye miradi mingi haswa ile ya hovyo.

2010 Kikwete akaleta Kitu kingine cha ajabu. Muhamed gharibu Bilali. Huyu ndio alikuwa ngariba mzoefu. Hata kwa kutumia mic sauti haitoki na haisikiki. Alikuwa mpole kama kuku mwenye mdondo. Ndio anashikilia rekodi ya kukata utepe toka Tanganyika iwe huru.

Japo ni msomi ila hakuwa na sifa ya uongozi.

2015 Magufuli akatuletea mdebwedo, ambao ulikuja kuokota dodo chini ya mwarubaini. Samia Suluhu Hassan. Hakufit kwenye nafasi ya umakamu wa rais na sasa amepwaya kabisa kwenye nafasi ya urais. Pamoja na kupwaya kwake huko naye akatuletea kituko kingine.

Emmanuel Nchimbi. Huyu jamaa tangu Samia aape pale dodoma hahaonekana zaidi ya mara nne kwenye shughuli za kuserekali. Muonekano wake haswa ile mimacho inanifanya niamini naye ni mzigo mwingine.

Ccm kwa nini haswa mnatuletea watu wa ajabu kwenye nafasi ya makamu wa rais?
Kapuku Lucas Mwashambwa unaitwa huku
 
Umenena vyema! Ni mtu wa msimamo. Siyo chawa. Anaijua CCM in and out. Huo ukimya una kishindo chake. Huyu si sawa na mnafiki Dr Mpango. Naamini Dr Nchimbi atatusaidia Watanganyika dhidi ya Uzanzibari unaotamalaki sasa hivi. Muda utaongea
Kama ukimya wake ni wa heri, na ikawe hivyo. Kama ni kwa uoga anaingia kwenye kundi la kina Bilali na shein
 
Sio kila mkimya na zobazoba ni fala...
Wewe. Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa msomi na kuwa kiongozi. Wale jamaa wakutoka zenji, Dr Ommary Ally Juma,Dr Shein, dr bilali ni wasomi. Ila hawana sifa ya kuwa kiongozi. Waliposwa kubaki na taaluma zao.
 
Back
Top Bottom