Hii nafasi ya Makamu wa Rais, mbona huwa tunaletewa watu wa ajabu sana?

Hii nafasi ya Makamu wa Rais, mbona huwa tunaletewa watu wa ajabu sana?

Hiyo ni nafasi ya kusubiria kiti kikuu kibaki wazi tu kabla ya muda uliopangwa jambo ambalo hutokea kwa nadra sana. Ukiangalia kiundani ni kupoteza pesa za umma tu kuwa na vyeo vya makamu wa rais na waziri mkuu kwa pamoja.
Tusiwe na makamu wa rais Ili rais akifa tuingie kwenye uchaguzi mkuu,unajua gharama ya uchaguzi?..naibu waziri nao tufute?
 
Kwenye hiyo orodha mtoe Emmanuel Nchimbi,toka enzi za Lowassa alionesha ni mtu wa msimamo ambae yupo tayari kusimamia kile anachoamini bila kujali nini kitampata.
 
Kwenye hiyo orodha mtoe Emmanuel Nchimbi,toka enzi za Lowassa alionesha ni mtu wa msimamo ambae yupo tayari kusimamia kile anachoamini bila kujali nini kitampata.
Kuwepo kwenye Serikali iliyoleta maafa kwa wananchi wake ndio msimamo?

Angesimamia kitu anachoamini kwa kutokubali kuwa mgombea mwenza ikiwa anafahamu taratibu hazikifuatwa.

Huu uzwazwa wa kuwashobokea watu ambao hawajali wananchi bali matumbo yao ndio unafanya hiki chama kiendelee kututawala siku zote.
 
Umenena vyema! Ni mtu wa msimamo. Siyo chawa. Anaijua CCM in and out. Huo ukimya una kishindo chake. Huyu si sawa na mnafiki Dr Mpango. Naamini Dr Nchimbi atatusaidia Watanganyika dhidi ya Uzanzibari unaotamalaki sasa hivi. Muda utaongea

Kigogo anadai kuwa jamaa kadhibitiwa.

Baada ya MO29 na Dada yake kuaga dunia alitaka kuungama. Si unajua tena maungamo ya Kikatoliki ...... Wenyewe hawataki kusikia hiyo kitu.
 
Kigogo anadai kuwa jamaa kadhibitiwa.

Baada ya MO29 na Dada yake kuaga dunia alitaka kuungama. Si unajua tena maungamo ya Kikatoliki ...... Wenyewe hawataki kusikia hiyo kitu.
Maneno ya vijiweni. Pale tumelamba dume Watanganyika
 
Back
Top Bottom