Uchaguzi 2020 Hii ndio awamu iliyofeli kuliko awamu zote zilizopita

Uchaguzi 2020 Hii ndio awamu iliyofeli kuliko awamu zote zilizopita

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Posts
240
Reaction score
767
Ziko sababu lukuki za kuonesha namna awamu hii ilivyofeli

1. Ikumbukwe walipoingia madarakani walituaminisha masuala ya wafanyakazi hewa na wanafunzi hewa wakatuambia na kiasi walichookoa na wakaendelea kutuaminisha awamu zilizopita zilikusanya kidogo embu tuone kuna ukweli.

(A) Awamu iliyopita hawakuchukua vyanzo vyama halmashauri, kwa wa machinga pia hawakuchukua sekta binafsi ndio ilikuwa injini sasa awamu hiii imechukua vyanzo vyote vya halimashauri lakini inaongoza kwa kukopa tena nje ya utaratibu Leo tycoon akitaka hata ajengewe sanamu yake pale chamwino DODOMA hahitaji baraka za bunge

(B) Mahakama kuwa karibu na serikali hasa kwenye kesi zinazokiuka haki rejea kesi ya Godbless Lema kesi ya viongozi wa chadema ama kesi iliyosomwa jana ya Mike Mushi na Melo nyuma ya hizi hukumu kuna mkono shinikizi kupitia mfumo

2. Hii ndio awamu inayooongoza kwa vitendo vya kikandamizaji tena hawajali rejea mauaji ya Kibiti ama kupotea kwa watu mbalimbali yu wapi msaadizi wa Freeman Mbowe ndugu Ben Rabiu Saanane wapi alipo Simoni Kanguye wapi alipo Azori Gwanda haya yote yanaonesha jinsi awamu hii ilivyoshindwa kulinda ustawi wa jamii

3. Kushambuliwa kiongozi wa upinzani mh Tundu Athipas Lissu katikati ya vipindi vya bunge na kuvuliwa ubunge kinyume cha sheria na pia kukosa hata kumnyima stahiki yake ya matibabu

Yote kwa yote hiii ndio awamu imeshindwa kuajiri kwa miaka zaidi ya minne imeshindwa kupunguza tatizo la ajira imepelekea vijana wengi kushiriki betting kwa kikukosa ajira

Mwisho huu ni mwaka wa uchaguzi ni lazima umma tukarejeshe utu uwajibikaji wa umma na demokrasia ishamiri tena kupitia sanduku la kura hiii ndo fimbo ya mnyonge ya kutetea utu wetu

#stayhome
#tunatakatumehuru
[emoji111]️


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani watu wa ufipa wategemee kupata laana kubwa kutoka kwa Muumba wa mbingu na nchi. Kwa nini?
Tangia tupate uhuru hakuna Raisi aliyewai kutukanwa mitusi mizito tena kama si amilijeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa taifa zima kama Mzee wa Msoga Ndugu yetu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. ( najua wamesahau)

Jamani walimshambulia huyu mzee wakamsurubisha hata juu ya msalaba, lakini yeye akawa kimya kama Yesu mzee wa watu.
Wakaanza kusema nchi hii inahitaji Rais na kuanza kutoa sifa ya raisi ajae.
Ukiangalia kila sifa waliyoitaja ilikuwa inamlenga Dr. John Pombe Magufuli.
 
Hilo la mwisho la kuajiri; kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi ili sekta binafsi ndio iendeshe uchumi hiyo kutoa ajira na kulipa kodi stahiki. Hivyo cha kuajiri ni kuangalia ajira za zimeongezeka katika sekta binafsi badala ya kuangalia tuu ajira serikalini.
 
Hilo la mwisho la kuajiri; kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi ili sekta binafsi ndio iendeshe uchumi hiyo kutoa ajira na kulipa kodi stahiki. Hivyo cha kuajiri ni kuangalia ajira za zimeongezeka katika sekta binafsi badala ya kuangalia tuu ajira serikalini.
Hata katika setka binafsi ajira zimepungua sana awamu hii. Mzunguko wa pesa mtaani ni mdogo sana.
 
Back
Top Bottom