Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye


Mkuu wangu, kama ungetaka watu wa "google", hata hiyo CV ya huyo mheshimiwa ilikuwa haina sababu ya wewe kuileta humu ndani ya JF. Yeye ni kiongozi mkubwa sana ndani ya CCM. Hivyo taarifa zake naamini lazima zitakuwemo katika tovuti yao ya chama.

Lakini kwa ubinadamu na wema wako kwa wana JF ukataka kuwarahisishia kuupata wasifu wa Bw. Nape, na ukauleta humu ndani ya JF. Basi endelea kuyajibu na hayo mengine kuhusu ufaulu wake.

Wahenga walisema "maji ukiisha yavulia nguo huna budi kuyaoga". Yaoge mkuu, usiyaogope kwani ninaamini unazo taarifa sahihi za huyo mheshimiwa.
Kwa mantiki hiyo, ondoa utata huu mkuu. Weka kila kitu wazi kuwakomesha hao wanaotaka kumchafua Mhe. Nape.
 
Akili ndogo (Nape Nnauye) inajaribu kutawala Akili kubwa (John J Mnyika) tunapelekwa pabaya na CCM
 

Mwanzoni nilifikiri hivyo - kwamba ni tarehe ya Graduation- lakini kwa historia ya mtajwa, iliyojaa umagumashi, ni vema na hilo likatolewa ufafanuzi. Hata jina tunaambiwa si lake. Kadhulumu haki ya mtanzania - masikini- ya kupata elimu kwa sababu tu ana uwezo. Hii ni kinyume kabisa na haki za binadamu, na ingefaa amefidie huyo kijana na Kinyirimba kwa wizi huu wa kihistoria.
 
Magumashi ya chaguzi yana mwanzo wake! Sasa huyu bwana alimiss qlf lakini akafanya exams za f six! kwenye fsix fake!
 
Acheni kutudanganya bana, hii sio CV hebu kajipange ndo uje upya... kama shule ya msingi tuu alisoma miaka 8 itakuwa sekondary??? alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India mh hii degiriii atakuwa nayo peke yake duniani Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma,Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma, hizi ni diploma au short cources......JIPANGE
Jaribu tena hapo umekwama li...CCM, Unadanganya cv we hujui kudanganya ni kosa kisheria!:nono:
 
hapo ndio watu wanapodondokewa na kitu chenye ncha kali.. tunaomba na wengine mnapokuja na siasa za elimu zenu msisahau kuonyesha kipengele hicho yaani KIWANGO CHA JUU CHA ELIMU YAKO, HATA KAMA STD SEVEN NDIO MAJAALIWA YAKO

Na aliifeka Masters yake in flat 1 year. Very sharp!
 
Akikupa hayo matokeo utakutana na kiambatanisho hapo chini, sasa jiulize F ya Maths na bado amesoma EGM
NAPE NNAUYE
DIV IV-29
KISW D, HIST D, GEOG D, ENG F, B/MATH F, BIOL D, CHEM D, PHY D, CIV F
Hivi anaruhusiwa mtu kusoma form 6 wakati ufaulu wake wa form 4 ulikuwa na average ya minus D?

Tanzania haiishi kunishangaza.
 
Jamani huyu mtu mpaka kusoma vidiploma inamaana matokeo yake hayakumruhusu kwenda digrii moja kwa moja! Kama anaweza aweke tokeo la form 4 na 6
 
Butimba TTC ni shule ya sekondari???????
Na hizo Diploma za mwaka mmoja mmoja ni certificates ama?????
Haya matango hamna kitu kajipange nae mje tena
 
napegwe jitu patel....
ahahahhhhhhahah......euuuuuuwiiiiiii.........napegwe j.p. ahhhhhhhhhhhhhhhhj....
 
Ukweli imebidi nisome mara mbili mbili kujiridhisha Butimba TTC,halafu kuna EGM:nono:

hamjamuelewa..ni hv katika vyuo vingi vya ualimu kuna kua na vituo vya private candidate(credit fighters) so mheshiwa alikwenda ku resit pepa alivyopata credt akafanya tena mtihani wa 4m6 kama private hapo butimba ttc...
 
tujulishe basi alipata ngapi form four
 
Nadhani alifanya kama private candidate butimba ttc hakukuwa na a level
 
Ili kukata mzizi wa fitna, tunaomba mdahalo kati ya mh.J .J mnyika na ndugu Nape. Nina uhakika hapo tutapata kujua mbivu na mbichi!
 

Tuambie hapo form 4 ulipata grade gani zilizokupeleka form 5??? Tujuze vizuri tuondoe ile tuhuma ya ufisadi wa elimu

 
Kama Nchi imefikia kuwa na vyuo mpaka vya kata ni kusema imefikia pazuri hivyo ni mfano mwema kwa Nchi kama Tanzania! Tukubaliane kwamba ndio ni vyuo vya kata, ila ni vya kata huko India na sio Tanzania! Lau chadema wakichukua nchi, wakafanikiwa kuufanya mfumo wetu wa elimu kuwa kama India yaani vyuo vikuu mpaka vya kata! Wakazalishwa kina Nape chekwaa mtaani katika vyuo hivo hapa hapa Tanzania haitakuwa jambo la kujivunia kweli kwa CDM? Au ndio yaleyale ya akutukanae hakuchagulii tusi? Binafsi sioni faida yoyote kuendelea kujadili Elimu ya Nape wala Mnyika! Ingekuwa vyema wasomi wetu mngejikita katika kujadili ni kwa namna gani jinamizi hili (la kufeli kwa vijana wetu) litaondoka hapa kwetu nyumbani Tanzania kwa kuchukua hatua hizi na zile! Hizi siasa zisitufanye tuwe wavivu wa kufikiri hata tukakosa muda wa kujadili mambo ya msingi yenye faida kwa Taifa letu!

Sasa jaman ukimaliza form six halaf ukaenda kusoma diploma maana yake uliliwa kichwa katika matokeo! Then ukaenda india kwa digrii, huko ndo kweny digrii za vyuo feki vya kitaa, kuna vyuo vya kata kama zilizovyo sekondary zetu za kata!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…