Matokeo ya Nape Nnauye ya Ordinary level secondary education ni Division TWO..,kwa anayetaka kujiridhisha anaweza ku-google mwenyewe NECTA matokeo ya Nsumba Secondary 1997. na hata kwa matokeo mengine pia ambayo Ni ya ndani ya Nchi na kuhusu matokeo ya chuo cha bangalore nayo yapo TCU.,ni jambo la kuuliza na kujibiwa.
Mkuu wangu, kama ungetaka watu wa "google", hata hiyo CV ya huyo mheshimiwa ilikuwa haina sababu ya wewe kuileta humu ndani ya JF. Yeye ni kiongozi mkubwa sana ndani ya CCM. Hivyo taarifa zake naamini lazima zitakuwemo katika tovuti yao ya chama.
Lakini kwa ubinadamu na wema wako kwa wana JF ukataka kuwarahisishia kuupata wasifu wa Bw. Nape, na ukauleta humu ndani ya JF. Basi endelea kuyajibu na hayo mengine kuhusu ufaulu wake.
Wahenga walisema "maji ukiisha yavulia nguo huna budi kuyaoga". Yaoge mkuu, usiyaogope kwani ninaamini unazo taarifa sahihi za huyo mheshimiwa.
Kwa mantiki hiyo, ondoa utata huu mkuu. Weka kila kitu wazi kuwakomesha hao wanaotaka kumchafua Mhe. Nape.