Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Nape ni msemaji wa CCM na Nape naye anamsemaji wake ndio huyo aliyeweka hiyo CV hapo so msishangae kwanini Nape hajaandika mwenyewe ilihali ni member humu, ni mgawanyo wa majukumu na wengine mkono uende kwa kinywa, ila hapo BUTIMBA TTC nadhani kijana unaweza ukawa _ fired nenda kajipange uje ufafanue vizuri.

Acha umbea wako,Tandale one ndiye nape mwenyewe, Full stop
 
Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;

  • Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
  • Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu "3" kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
  • Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
  • Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
  • Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa –Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
  • Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
  • Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe.
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika "thesis" iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)

Ha ha ha hebu tueleze vizuri huko Butimba TTC alikuwa kama mwalimu au PC yaan Private Candidate? Mtahangaika sana mkuu, Nape hajwahi soma Butimba kwani sisi ndiyo wenyeji wa Butimba na mimi personally nimekuwa nikisoma naye Nsumba Sekondari. Njoo na CD nyingine>
 
Dah kumbe upo vizuri kaka, ila sasa kule kuropoka ropoka kunatoka wapi? Wakati unaelimu nzuri tu.
 
Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;

  • Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
  • Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu “3” kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
  • Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
  • Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
  • Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa –Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
  • Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
  • Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe.
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika “thesis” iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)

Kwa CV hii alitakiwa awe Katibu mwenezi wa Kata.
 
huyu hafai hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji maana anaweza leta maafa kwa uropokaji wake.
 
Du, mbona CV imekaa kama historia ya kwenye mazishi. Ni mtazamo tu.
 
Jamaa ni Msanii kwelikweli. Butimba TTC Sec. School hajawahi kuwa na A Level......
mimi ni Mwalimu hapa.. Kama ndo siasa yenyewe hii. basi kwaherini..
 
"Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC'
Kaandae upya hii cv ya kuforge, 1998-2000 High School + kuhitimu Butimba TTC ambako ni chuo cha ualimu!!!!!!!!!!!
 
Diploma gani ya ualimu alisoma at the same time advanced level?
Cv gani hii chafu,hadi kichefuchefu.
 
Duh. Jamaa kwa miaka 2 kapata diploma 2 tofauti. Walah elimu ya bongo ingekua hivi watz wote wangekuwa wasomi
 
vipi cv za hawa hapa chini???
1.mbowe
2.msigwa
3.sugu
4.vicent nyerere
5.msabaha yule dada wa viti maalum kutoka znz
6.chiku abwao

nawasilisha
 
Jamaa ni Msanii kwelikweli. Butimba TTC Sec. School hajawahi kuwa na A Level......
mimi ni Mwalimu hapa.. Kama ndo siasa yenyewe hii. basi kwaherini..
vyuo vya ualimu vyote hapa nchini ni vituo vya mtihani kwa watahiniwa wa kujitegemea. kawadanganye wanao nyumbani
 
Back
Top Bottom