USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 12,213
- 28,916
Kwenye ulimwengu ambapo kila dini inahubiri utakatifu na maisha ya ucha Mungu, kuna imani moja kutoka nchini India inayovuka mipaka yote ya akili ya kibinadamu—Ujaini (Jainism). Hii si dini ya kawaida; ni nidhamu ya kiwango cha juu cha kiroho ili uweze kuwa mtakatifu kweli.
Wajaini wana fuata sheria kali sana, Swala tano wakasome, kama ifuatavyo.
Hawatagusa Nyama Kabisa: Wajaini wote ni vegetarian wakali sana. Hawali nyama, samaki, au mayai.
Hawali Mimea Inayoota Chini ya Ardhi: Hawali kitunguu saumu, kitunguu maji, wala Viazi Mviringo/Karoti. Sababu? Kung'oa mmea ardhini kuua kiumbe kizima, na pia kuna viumbe vidogo vingi vinavyouawa ardhini wakati wa kuchimba.
Hawali Usiku: Wajaini wengi hawali wala kunywa baada ya jua kuzama ili kuepuka kula kwa bahati mbaya wadudu wanaovutiwa na mwanga usiku.
Ulinzi wa Wadudu: Watawa wa Kiujaini hufagia chini wanapotembea ili wasikanyage wadudu, na wengine huvaa barakoa midomoni ili wasimeze viumbe wadogo waliopo hewani kwa bahati mbaya.
Lakini kipimo cha juu kabisa na cha kutisha zaidi cha kujitenga na tamaa za dunia katika Ujaini ni ibada ya kifo inayojulikana kama Santhara (au Sallekhana).
Hiki si kitendo cha kujiua kwa hasira—ni maamuzi ya hiari na ya utulivu ya kuacha kula na kunywa taratibu hadi mauti yanapowadia!
Mchakato huu wa kutisha unafanyika hatua kwa hatua:
Mhusika (mara nyingi akiwa mzee, mtawa, au mgonjwa asiye na tiba) humwomba kiongozi wa kiroho kibali ili kuthibitisha kuwa akili yake haina huzuni wala majuto. Akishaidhinishwa, huomba msamaha kwa kila kiumbe hai duniani alichowahi kukikosea, na kuwasamehe maadui zake wote.
Mtu huyo haachi kula ghafla. Mchakato unaanza kwa kupunguza vyakula vizito kwa wiki kadhaa, akibakiwa na vinywaji vyepesi pekee kama maji ya moto.
Hatimaye, akili inapofikia utulivu wa mwisho, anacha hata kunywa maji. Mwili unanyauka na kukauka taratibu huku akiwa amezungukwa na familia inayomsomea sala za kumsindikiza.
Kwa kua ulikua huli kwa muda mrefu inatakiwa ukifa, mwili wako usioze, unyauke tu, na kukauka, ukikutwa umeoza, umekosea MASHARTI na huhesabiki kama mtakatifu.
Walo wai kuvuka mtihani huu ni wachache sana na wana abudiwa kama watakatifu.
Serikali ya india iliwai kuingilia kati na kutaka kufuta hii kitu ya kuacha kula, ila waliwashinda Mahakamani na kufaulu kuendelea nayo