MZIMU
JF-Expert Member
- Apr 29, 2011
- 4,058
- 1,373
1. Ndoa yao ina miaka 65.
2. Hawana skendo yoyote.
3. Mtoto wao wa kiume ambae ni Mrithi wa Ufalme kwa mujibu wa katiba ya nchi yao, mpaka sasa ana miaka 65, akimsubiria mama yake afe ndio awe mfalme. Na ukoo unarekodi ya kuishi umri mrefu kupita maelezo, maana Mama wa huyu Malikia wa sasa aliishi Karne moja. Sasa Huyu dogo kazi anayo.
Huyu mtoto, tofauti sio kama angekua mtoto mwengine, hana presha, hana tamaa ya Kua mfalme, halalamiki, ana onyesha heshima na Mapenzi takatifu kwa wazazi wake hao. Anasubiria tu, anazeeka katika kusubiri, mpaka watu wanasema hata mama yake akifa, asipewe ufalme bali apewe mjukuu ambae ni Mwanae yeye Charles.