Hii ndio ilikuwa “Ze Comedy” ambayo ilisamamisha nchi ilipofika saa moja jioni

Hii ndio ilikuwa “Ze Comedy” ambayo ilisamamisha nchi ilipofika saa moja jioni

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Screenshot_20250302-103249.png

Hapa ndipo tulipopata misemo mingi sana kama ule wa kudadadeki (Nafikiri joti aliutoa katika msemo wa "kulaleki" ukikuwepo tangu 90s), umefulia, etc

miondoko ya aina yake, hapa ndipo tulipogundua wasanii walivyoiba style za wasanii wa nje then joti akawa anawa expose, mpoki kumuiga marehemu komba,

Miaka hio masanja anawadiss beki tatu na ndugu waliotembelea kusalimia nyumbani kwa watu na hawataki kurudi kwao 😂😂

HAKIKA HAWA JAMAA NI TUNU YA TAIFA
 
"Nikushukuru na wewe unaenitazama ukiwa sebuleni kwa shemeji yako, dada yako ameolewa na wewe umeenda kukaa kwa shemeji yako, yaani wote wawili mmeolewa"

Baridi inayopiga hapo nyie achaaa!!! 😄 .

Unakuta shemeji nae yupo anaangalia.

Halafu mazingira kama haya unakuta vile vitoto age ya 3 -6(vi anko) vilikua vinamfuatisha masanja yale maneno, akifika kwenye hicho kipande "NIKUSHUKURU WEEWEE!!(hawajui ni kiasi gani wanakusurubu rohoni)

Ze comedy ilipokua inafikia hapa nilikua napata wakati mgumu sana 🤣

Hapo unajikuta baridi inakuingia mpaka kwenye mifupa, kesho ni lazima uamke mapema sana kwenda kutembeza bahasha kwa hasira maofisini, ila napo unajikuta holaaaa no job.

Jioni unarudi kwa mmeo. 😄 🤣 😂
 
View attachment 3255573

Hapa ndipo tulipopata misemo mingi sana kama ule wa kudadadeki (Nafikiri joti aliutoa katika msemo wa "kulaleki" ukikuwepo tangu 90s), umefulia, etc

miondoko ya aina yake, hapa ndipo tulipogundua wasanii walivyoiba style za wasanii wa nje then joti akawa anawa expose, mpoki kumuiga marehemu komba,

Miaka hio masanja anawadiss beki tatu na ndugu waliotembelea kusalimia nyumbani kwa watu na hawataki kurudi kwao 😂😂

HAKIKA HAWA JAMAA NI TUNU YA TAIFA
Hii comedy ndiyo iliyatoa haya majamaa maana kabla ya hapo yalikuwa yamezeeka! Hao wengine mbona hawasikiki? Vengu na mwenzake!
 
"Nikushukuru na wewe unaenitaza ukiwa sebuleni kwa shemeji yako, dada yako ameolewa na wewe umeenda kukaa kwa shemeji yako, yaani wote wawili mmeolewa"

Ze comedy ilipokua inafikia hapa nilikua napata wakati mgumu
😂😂
 
View attachment 3255573

Hapa ndipo tulipopata misemo mingi sana kama ule wa kudadadeki (Nafikiri joti aliutoa katika msemo wa "kulaleki" ukikuwepo tangu 90s), umefulia, etc

miondoko ya aina yake, hapa ndipo tulipogundua wasanii walivyoiba style za wasanii wa nje then joti akawa anawa expose, mpoki kumuiga marehemu komba,

Miaka hio masanja anawadiss beki tatu na ndugu waliotembelea kusalimia nyumbani kwa watu na hawataki kurudi kwao 😂😂

HAKIKA HAWA JAMAA NI TUNU YA TAIFA
Joti mwenyewe alimkopi martin lawrence ule mwendo wake,kudadeki lipo tu tangu 90
 
"Nikushukuru na wewe unaenitaza ukiwa sebuleni kwa shemeji yako, dada yako ameolewa na wewe umeenda kukaa kwa shemeji yako, yaani wote wawili mmeolewa"

Ze comedy ilipokua inafikia hapa nilikua napata wakati mgumu
Hawakua na busara
 
Wakuvanga alikuwa anamuiga marehemu Lowassa na Kikwete.
Mpoki alikuwa anamuiga marehemu Komba.
Vengu alikuwa anamuiga marehemu Mrema.
Masanja alikuwa anamuiga Mizengo Pinda.
Bila kuwasahau Joti na Mac Regan. Joti, Masanja na Mpoki ndio walikuwa wanafunika zaidi hasa Joti. Akiigiza mzee, Mtoto, Mwanamke au mpemba kote huko alikuwa anamudu.
Kila likitokea habari kubwa ya kitaifa iwe ya kimichezo au ya kisiasa wao watailezea ki-comedy zaidi.
Majina ya watu walikuwa wanayabadilisha kuweka katika hali ya kuchekesha, mfano Zito Kabwe walimwita Nyepesi Mbabe.
Clips zangu bora zaidi kutoka kwao ni video ya wimbo wa Boss wa Feruz na ile ya marehemu Lowassa anacheza wimbo wa Banjuka tu.
Ratiba yao ilikuwa ni kila alhamisi saa moja usiku EATV.
Ni kweli ikifika muda huo nchi ilikuwa inasimama kupisha jambo lao, ilikuwa ni kama mechi ya Simba na Yanga inapochezwa.
 
Back
Top Bottom