Hii ndio ilikuwa “Ze Comedy” ambayo ilisamamisha nchi ilipofika saa moja jioni

Hii ndio ilikuwa “Ze Comedy” ambayo ilisamamisha nchi ilipofika saa moja jioni

View attachment 3255573

Hapa ndipo tulipopata misemo mingi sana kama ule wa kudadadeki (Nafikiri joti aliutoa katika msemo wa "kulaleki" ukikuwepo tangu 90s), umefulia, etc

miondoko ya aina yake, hapa ndipo tulipogundua wasanii walivyoiba style za wasanii wa nje then joti akawa anawa expose, mpoki kumuiga marehemu komba,

Miaka hio masanja anawadiss beki tatu na ndugu waliotembelea kusalimia nyumbani kwa watu na hawataki kurudi kwao 😂😂

HAKIKA HAWA JAMAA NI TUNU YA TAIFA
Noma sana
 
Wakuvanga alikuwa anamuiga marehemu Lowassa na Kikwete.
Mpoki alikuwa anamuiga marehemu Komba.
Vengu alikuwa anamuiga marehemu Mrema.
Masanja alikuwa anamuiga Mizengo Pinda.
Bila kuwasahau Joti na Mac Regan. Joti, Masanja na Mpoki ndio walikuwa wanafunika zaidi hasa Joti. Akiigiza mzee, Mtoto, Mwanamke au mpemba kote huko alikuwa anamudu.
Kila likitokea habari kubwa ya kitaifa iwe ya kimichezo au ya kisiasa wao watailezea ki-comedy zaidi.
Majina ya watu walikuwa wanayabadilisha kuweka katika hali ya kuchekesha, mfano Zito Kabwe walimwita Nyepesi Mbabe.
Clips zangu bora zaidi kutoka kwao ni video ya wimbo wa Boss wa Feruz na ile ya marehemu Lowassa anacheza wimbo wa Banjuka tu.
Ratiba yao ilikuwa ni kila alhamisi saa moja usiku EATV.
Ni kweli ikifika muda huo nchi ilikuwa inasimama kupisha jambo lao, ilikuwa ni kama mechi ya Simba na Yanga inapochezwa.
😂😂😂
 
Brain behind alikuwa mnyama Seki jamaa alikuwa anajua sana huyu nashangaa amejitenga sana na tasnia
 
Back
Top Bottom