Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uchawa umewamalizaView attachment 3255573
Hapa ndipo tulipopata misemo mingi sana kama ule wa kudadadeki (Nafikiri joti aliutoa katika msemo wa "kulaleki" ukikuwepo tangu 90s), umefulia, etc
miondoko ya aina yake, hapa ndipo tulipogundua wasanii walivyoiba style za wasanii wa nje then joti akawa anawa expose, mpoki kumuiga marehemu komba,
Miaka hio masanja anawadiss beki tatu na ndugu waliotembelea kusalimia nyumbani kwa watu na hawataki kurudi kwao 😂😂
HAKIKA HAWA JAMAA NI TUNU YA TAIFA
Kweli kabisa " kudadeki" lipo kitambo ila " kudadadeki" ndio limekuja baadaeJoti mwenyewe alimkopi martin lawrence ule mwendo wake,kudadeki lipo tu tangu 90
🤣 .Ulikuwa kwa shemeji yako mkuu?
Daah pole sanaa mwamba umeandika kwa uhalisia sanaaa ... ila naamini sasa hivi Mungu alishafungua milango mingine fresh kabisa."Nikushukuru na wewe unaenitazama ukiwa sebuleni kwa shemeji yako, dada yako ameolewa na wewe umeenda kukaa kwa shemeji yako, yaani wote wawili mmeolewa"
Baridi inayopiga hapo nyie achaaa!!! 😄 .
Unakuta shemeji nae yupo anaangalia.
Halafu mazingira kama haya unakuta vile vitoto age ya 3 -6(vi anko) vilikua vinamfuatisha masanja yale maneno, akifika kwenye hicho kipande "NIKUSHUKURU WEEWEE!!(hawajui ni kiasi gani wanakusurubu rohoni)
Ze comedy ilipokua inafikia hapa nilikua napata wakati mgumu sana 🤣
Hapo unajikuta baridi inakuingia mpaka kwenye mifupa, kesho ni lazima uamke mapema sana kwenda kutembeza bahasha kwa hasira maofisini, ila napo unajikuta holaaaa no job.
Jioni unarudi kwa mmeo. 😄 🤣 😂
Sekioni David last time alikua mtangazaji habari hapo hapo ITV au EATV sikumbuki vizuri, wakati jamaa wana~hit na Ze~comedy yeye alikua anatangaza habari, km ulivyosema ilikua inasemekana show ni ya kwake. Baada ya hapo sijamsikia tena.Brain behind alikuwa mnyama Seki jamaa alikuwa anajua sana huyu nashangaa amejitenga sana na tasnia
EATIV au EATVEATIV, sio ITV
Hili swali ndio litarefusha thread sasaHivi Vengu yupo wapi kwa sasa?
Duuuh!!! Sasa toka kitambo hiyo mpaka leo ukae kwa shemeji 🤣 .Daah pole sanaa mwamba umeandika kwa uhalisia sanaaa ... ila naamini sasa hivi Mungu alishafungua milango mingine fresh kabisa.
Watu wakitengana ndio utajua nani alikua anabebwa na nyota za wenzake.Vengu alikuwa anabebwa. Kama alivyosema ephen_ ni kweli pengo lao halizibiki. Nao walizingua walipojiingiza kwenye ugomvi wa Mengi na Manji.
JPm alikuwa msanii sana,kuna kipindi alituletea idadi ya Sangara wenye mimba!🥴Kuna clip moja masanja anampigia simu mheshimiwa the late Magu enzi akiwa waziri wa uvuvi, anataja idadi ya samaki wote dah inachekesha sana.
masanja: mheshimiwa we unajidai unajua haya pegere wako wangapi?
magu: pegeree wako bilioni 5 milioni 4 laki mbili mia na 7(in magu voice)
huwa nikikumbuka nacheka huku nalia 🙁