Hii ndio Interview iliyoifanya dunia ifahamu uwepo wa huyu kiumbe

Hii ndio Interview iliyoifanya dunia ifahamu uwepo wa huyu kiumbe

Huwa siwajali sister. Mi naishi maisha yangu ndo maana hata mtu akisema haamini i dont bother. Sababu si jukumu langu kumuaminisha. Mi natoa tu taarifa kuamini au kutokuamini ni juu ya msomaji. Hainiathiri chochote.
Mzeet wa ma tea.....
next time chemsha birika kubwa kabisa...
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Anasema hii ndiyo interview iliyomfanya awe maarufu na ajulikane. Sasa kwa vigezo alivyoonesha, ni wazi kama alikuwa hajulikani before, basi most probably hakuwa anaishi hapa duniani.
 
Watu wenye vigezo kama hivyo huwa hawapotezi time kwa masuala ya kazi wala nini, achilia mbali interview. Sasa huyu virtual graduate yeye anasema yuko ^humble^ ndiyo maana anataka kufanya kazi na hao jamaa zake. Halafu anaishi dunia ya tatu --- wakati dunia hii ingali moja tu. Dunia ya pili na tatu, labda ideas za watu wa London & Washington huko
 
Sijawahi kuona interview unaingia kabla ya kuwasilisha Siivii. Hii ni incredible and stunning even.
 
Faza we baki na kazi za mwezini tu, huko mbinguni kazi zinepungua idadi maana hatanamba moko wetu hapa jamhurini keshaziwahi mbili chap.....kachagua kabisa kama siyo kupiga deki basi kuongoza malaika!!!
 
Nina maswali 5 tafadhali naomba kujibiwa!
Swali la kwanza! Cheti chako cha mwisho ulichofuzu, ulisomea nini na kwa mda gan?
 
Leo mmoja ya ma profesa watano ambao walikuwepo kwenye Interview panel waliyonifanyia amenipigia simu kunisalimia.

Nakumbuka siku hiyo nimeitwa kwenye interview kulikuwa na watu 10. Maprofesa 5, Phd Holders 3 na ma CEOs wa Makampuni makubwa Duniani 2.

Interview ilianzia Kenya,ikaenda South Africa,Ikaenda Egypt, ikahamia Ulaya na Marekani.

Pale Kenya ndo walinichoka. Waliniuliza kwa nini tukuchague wewe na si wengine.

Niliwarekebisha kwanza. Nikawaambia siyo wao wanichague. Mimi ndo niwachague kufanya nao kazi.

Jamaa walishtuka Mmoja akauliza kwa nini. Na kumbuka hili ni shirika la Kimataifa la fedha Duniani.

Nikawaelezea CV yangu ni kubwa sana. Prof mmoja akasema nimpelekee. Nikampelekea. Akanambia "Siyo kitabu nipe CV yako" nikamwambia ndo hiyo. Akasema hapana. Akafungua akakuta kuna pages 200.

Wakasema niwape muda wajadiliane mambo. After 10 mins wakaniita wakanambia wameamua nijielezee.

Nlianza jielezea saa 3 ile mpaka saa 6 nawaeleza Makampuni ambayo nimefanya nayo kazi na pia Elimu yangu. 3 hours wakanambia nipumzike kwanza nao wapate break.

Baadaye waliponiita wakasema nimebakiza kama muda gani. Nikawaaambia masaa kama 6 hivi ndo nimalize. Wakanijibu niachane nayo wameshanielewa.

Basi nikawaambia waniulize maswali.wakawa hawana wanatizamana tu usoni na kila mtu naona alikuwa busy kuandika nliyokuwa naongea. Nlikuwa kama nawapiga lecture.

Saa zima nawasubiri waniulize maswali wanategeana. Nikawaambia basi niwaulize mimi maswali. Wakagoma kabisa.

Wakasema suala langu niende nikajadiliane na watu wa South Africa, kule wakasema niende Egypt kule wakasema niende nchi kadhaa za Ulaya, wakanisukumia China,wakanirudisha USA. Huko ndo wakaniuliza kwa nini kwa ile CV nmeamua kufanya kazi nao maana wanaona kama hakuna Shirika Duniani linaweza ni hire.

Nikawaambia ni mapenzi tu kutaka isaidia Dunia wakaniomba niwatajie nataka nilipwe Usd ngapi. Ila wakanisihi sana nisije nikatamka kubwa mpaka wakanikosa.

Basi ndo Kuajiriwa. Sikai sana Ofisin mara ILO wanataka kunitumia, mara IMF mara WHO, mara UNHCR, mara UN, mara OAU yaani nimejikuta tu kila sehemu wananitaka. Ukiacha Apples , Bill Gates, Warren Buffet, Ali Baba, Amazon ambao wao hutaka nifanyie tu Consultation. Wananilipa kwa sekunde.
Matajiri na baaadhi ya wasomi wakubwa Duniani wananambia bwana mdogo kwa hii CV labda ukaombe kazi Mbinguni tu. Huku Duniani ni kama tunakupunja. Halafu mpaka kitakosekana cha kukupa changamoto.

Huwa siwajibu kitu. Natabasamu tu coz nipo very Humble. Leo wananishangaa kuwa Why nakuja ishi nchi ya Dunia ya Tatu. Wakati ngeungana na watu flani flan tungeweza hata enda Ishi Mwezini huko. Au hata Mbinguni.
Ndo matokeo ya kunyoa kiduku popote penye nywele.Muulize Mwajuma au Jane watakueleza au kaka yao Juma au Mwakimbotilesamesha.
 
Bingw wa fix

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Usikute huyu jamaa ndio yule anaebandika mabango ya "Sultan mzibua vyoo"
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Back
Top Bottom