Mimi nimekwazika tu uliposema kuwa jukwaa la mahusiano lina wachangiaji wengi kwa kuwa nyanja hii inamgusa kila mtu.... Huu ni ukengefu, wa upofu na upogo na ni upotoshaji wa kiwango cha juu kabisa!
Hilo jukwaa linaitwa kwa kifupi MMU, yaani mahusiano, mapenzi na urafiki lakini kiuhalisia linajikita zaidi kwenye Mapenzi na Mahusiano. Nataka nikuambie kwamba nina ushahidi wa watu kadhaa, watu wazima ambao katika maisha yao hawajawahi ama hawajihusishi kabisa katika mahusiano au mapenzi.
Lakini, unaposema kuwa hili jukwaa linamgusa kila mtu kwani siasa haimgusi kila mtu, maamuzi ya kisiasa yanapitishwa bungeni hayamgusi kila mtu? Maagizo yanayotolewa na wanasiasa hayamgusi kila mtu?
Kwani jukwaa la uchumi halimgusi kila mtu? Mfumuko wa bei ukitokea haumgusi kila mtu?
Ndugu yangu
KENZY , sababu pekee inayofanya hilo jukwaa liwe na watu wengi ni kwa kuwa binadamu wengi, hasa hasa sisi ngozi nyeusi tunawaza sana mapenzi na ngono kuliko kitu kingine.
Siku nyingine unapoandika mada, jiepushe na upotoshaji.