Hii ndio mifumo bora ya kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa ufanisi mkubwa na faida kubwa

Ahsante sana kwa mchango wako mkuu. Kama Rais anapitia hapa hatuna budi kumwomba walau apitie mawazo yetu.
 
Katika ushauri wako kuna mikanganyiko mingi sana, na pia maelezo ni marefu sana,ila umezungumzia point tatu .
Ila kwa ufupi ni kwamba
Point kubwa uliyoizungumzia ni
Udart iendeshwe kwa mfumo wa hisa,na iwe taasisi huru
 
Kuna watu wengi wanaongelea mradi wa mwendokasi bila kujua Nia na madhumuni ya kuanzishwa.
Mradi huu ulianzishwa baada ya kubainika serikali ilikuwa inapoteza pesa nyingi kwa sababu ya watu kutumia muda mwingi kwenye foleni badala ya kuzalisha.
Duniani kote mwendokasi inaendeshwa na serikali kwa sababu mradi hauingizi pesa moja kwa moja Bali inapofikisha watu kwa haraka wanazalisha na serikali inapata mapato kupitia Kodi ya mapato wanayozalisha.
Mwendokasi inatakiwa iondoke hata ikiwa na mtu mmoja kitu ambacho mwekezaji binafsi hawezi kufanya.
Uingereza waliwahi kukabidhi mradi kwa mtu binafsi lakini walimnyang'anya baada ya mfupi sababu alikuwa haondoi Basi Hadi lijae.
Tatizo la nchi hii ni kuteua watendaji wabovu ambao Wana uwezo mdogo na pia kuihujumu huu mradi ili viongozi waweze.kumiliki kupitia uwekezaji binafsi.
 
Katika ushauri wako kuna mikanganyiko mingi sana, na pia maelezo ni marefu sana,ila umezungumzia point tatu .
Ila kwa ufupi ni kwamba
Point kubwa uliyoizungumzia ni
Udart iendeshwe kwa mfumo wa hisa,na iwe taasisi huru
Mkuu shukrani kwa kuona pale ambapo sijaeleweka vyema. Na shukrani kwa kutoa mwongozo mwepesi.
 
Si unamuona mwenye akili hapa ametoa Maoni?Bwana Meneja wa Makampuni Unaonaje Tukiuchukua Mradi tuuendeshe?
UDART wajitahidi kufuata ushauri kila kitu kitakwenda sawa. Kila kitu ni kufuata kanuni na taratibu tu. Huduma nzuri kiwe kipaumbele cha kwanza ndio faida ifuate.
 
Kwa ufupi ukimpa mwekezaji wape kampuni zaidi ya mbili ili waendeshe Kwa ushindani na kuwapa ratiba
 
Umeniongezea kitu [emoji2935]
 
Tatizo kubwa la Mwendokasi ni nauli yenye uhalisia. Mradi ulipokuwa unaandikwa mwaka 2010-13, ulibase kwenye NAULI ya Tsh 3,000 kwa roud trip. Yaani Mbezi Mwisho- Gerezani - Mbezi Mwisho.

Haya ndiyo mahesabu yaliyotumika kukopa fedha za kununua mabasi kutoka Benki ya NMB na SIMON GROUP.

Sasa nauli inayotolewa ni kama Tsh 1,850 tu kutoka Mbezi Mwisho hadi Ferry na kurudi.

Je hiyo tofauti ya Tsh 1,150 anailipa nani ?

Na kwa vile hiyo Tsh 1,150 haipatikani matokeo yake ni UDART kushindwa kukarabati mabasi yake na kununua mapya. Gharama kubwa ya UDART ni katakana ya kutengeneza mabasi. NAULI WANAYOKUSANYA SASA HAITOSHI KUENDESHA KAMPUNI kwa ufanisi.

Hata hao wazabuni wanaotafutwa kama hawataongezewa nauli, hawawezi ku operate kwa nauli ya Tsh 1,850


USHAURI:
Kwa vile usafiri wa mjini ni huduma na si biashara, Serikali utafute namna ya kuipata hiyo tofauti ya Tsh 1,150 kutoka kwenye vyanzo vingine na kuiongeza kwenye nauli ya Tsh 1,850

Hqta majiji ya Ulaya Magharibi kuna subsidy ambayo municipal councils zina support urban transportation
 
Ungesoma ripoti ya cag alisema mwendokasi wangeokoa pesa nyingi Kama wangetumia mfumo wa gesi, kwanini mpaka Sasa hawajatumia huo mfumo wa gesi.
 
Ungesoma ripoti ya cag alisema mwendokasi wangeokoa pesa nyingi Kama wangetumia mfumo wa gesi, kwanini mpaka Sasa hawajatumia huo mfumo wa gesi.
Hiyo ni moja ya solutions ya kupunguza gharama. Lakini haiwezi kusababisha ukafuta hiyo tofauti ya nauli iliyopitisha mradi na nauli inayotumika sasa
 
Hiyo ni moja ya solutions ya kupunguza gharama. Lakini haiwezi kusababisha ukafuta hiyo tofauti ya nauli iliyopitisha mradi na nauli inayotumika sasa
Lakini watanzania hawana tatizo na mambo ya nauli wakuu. Nauli ilisha ongezwa lakini bado mpaka sasa watanzania wanapenda kutumia mwendokasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…