Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Jiji la dar ni ilala, zilizo baki ni manispaa, uzuri ukisoma andiko lake hapo juu utaona dar ni mjumuiko wa halmashauri zote

Mwanza sijui

Mbeya haipo hivyo wala Arusha sababu kuna mnyumbuliko wa halmashauri zingine

Tunapo chambua hizi Halmashauri au kuamua kuzinyumbua tuweke mnyumbuliko huo sababu kila Halmashauri ina mamlaka zake kwa kuzingatia jiografia mamlaka nk

Ni jambo ambalo sio sawa kwa kushindwa kuweka sawa data za kila mamlaka kwa kuzingatia vyanzo vyake vya mapato vya ndani...

Ukiulizwa mapato ya Halmashauri ya ubongo ni kiasi gani? Una weza kutuambia?
 
Sasa pesa za TRA hazina faida kwa Halmashauri husika tofauti na hizi wanazokusanya na kutumia wenyewe

Upigaji uko kote kote hasa Halmashauri maana wanakusanya wenyewe.Ujue Halmashauri zinatakiwa zijitegemee badala ya kusubiria ruzuku kutoka serikali kuu
 
Nimenyumbulisha kama ulivyoshauri
 
Serikali inachofanya ni unfair game. Kama ingekuwa inaruhusu halmashauri zikusanye kodi zenyewe then Percent fulani iende central gov ingekuwa sawa. Lakini yenyewe inakaba vyanzo vyote matokeo yake Wilaya zenye rasilimali chache zinasuffer sana. Kwa sababu ni kama zimekatwa mikono. Ila cha ajabu wilaya ambazo mapato ya ndani siyo makubwa wananchi wake wana afadhali sana ya kimaisha. Rejea takwimu za taifa za hali ya umasikini nchini utaelewa nachokwambia
 
Sawa lakini umewahi kufika katika pori hilo la kagera nkanda ukafahamu mkulima was hali yachini analima hekali ngapi, huwa ni kuanzia 5 mpaka 300 hecter, na kusingekuwa na mazao ya biashara wasingefungua soko la mazao tu sijui unafahamu Hilo, Burundi, Congo na Rwanda wanategemea nafaka kutoka katika soko hili mpya la mazao, njoo uone store za mazoa mfanya biashara was chini anagunia Kama 300 , Kuna sehemu moja inaitwa heru juu miti hii ya kupandwa ndio biashara imewatajirisha ghorofa zimeanza kujengwa kwa Kasi, vip kipato kitakuwa hakitoshi au,
 
Hifadhi za utalii huwa hazitoi mirabaha kama hiyo migodi?
 
Sio Top Ten ni Top Five
 
Mkuu Mufindi hakuna pesa kama zamani, marehemu Magufuli amepavuruga sana.
Kuna jamaa alinipa ABC ya jinsi wanavyofanya biashara ya miti ya nguzo kupeleka mgololo nilistaajabu sana. Biashara ya pesa balaa. Bado chai na mbao. Lakini siku nyingi wilaya hii inafanya vizuri.

Jiwe hakupenda watu kuwa na hela kabisa.
 
Kuna jamaa alinipa ABC ya jinsi wanavyofanya biashara ya miti ya nguzo kupeleka mgololo nilistaajabu sana. Biashara ya pesa balaa. Bado chai na mbao. Lakini siku nyingi wilaya hii inafanya vizuri.

Jiwe hakupenda watu kuwa na hela kabisa.
Mufindi kuko vizuri sana mkuu, sema tu marehemu alivuruga mambo mengi sana. Miti saa hizi imeshuka bei hivyo wajanja hawavuni wanasubiri bei ipande juu tena.
 
Kwani wakijenga vijijini kwao wanakuwa wamefilisika kiasi cha kushindwa kujenga mjini? We kama hupendi maendeleo ya kijijini kwenu hilo ni tatizo lako usitake kuamlia watu wengine! Mjini hapaendelezwi na wenyeji tu bali watu kutoka sehemu mbalimbali. Mfano Morogoro mjini hakuna mluguru anayemiliki kitu cha maana infact waluguru wote wamewaachia mji wageni wao wanajilimia magimbi yao huko milimani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…