Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Arusha haina rasilimali za maana, Hivi unafahamu Manyara ndio ina rasilimali nyingi kama mkoa anzia mererani kumbuka iko manyara, hivo tanzanite haipo Arusha, ongezea na mbuga zilizoko manyara hivo Arusha ukitoa viwanda hawana kitu kingine kipya
Mkuu wewe kubali angalia hapo hakuna Halmashauri hata moja kutoka mkoa wa Manyara ime appear kwenye list,hizo rasilimali zinasaidia wapi?

Hata kwenye mapato ya TRA Manyara kapigwa mbali na Arusha
 
Hii haihusiani na ubora wa maisha katika halmashauri hizo, wala kipato cha mtu binafsi katika halmashauri husika. Kuna halmashauri zenye mapato makubwa kwasababu kuna mradi mmoja mkubwa pale. Mfano Mlimba kuna mashamba ya walowezi ya mitiki, ni makubwa na ndio chanzo kikubwa cha kodi. lakini kipato binafsi na hali ya maishi iko chini mno!
Inaweza kuwa haiakisi moja kwa moja lakini ni kuashiria tosha maana huo mradi na uhakika haulipi hata robo ya hayo mapato ya Mlimba DC
 
Ifuatayo ni orodha ya Miji na Halmashauri 36 ambazo watu wake Wana kipato cha Uhakika na kuwa na purchasing power inayotoa fursa ya uhakika wa biashara kwa Tanzania.
Orodha imehusisha Halmashauri zenye mapato yanayoanzia shilingi za Tanzania bilioni 3.5 kwenda juu.

Orodha hii imetokana na makusanyo ya ndani ya kila Halmashauri kiutoka kwenye vyanzo vya mapato vya Halmashauri ambavyo ni shughuli za kawaida za wananchi kutoka Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mapato hayo ni nje ya vyanzo vinavyokusanywa na TRA na wakala zingine za.serikali.

Kama wewe ni mfanyabiashara hii itakuwa picha halisi ya uchaguzi wa sehemu ya kuwekeza.

1.Dar (Na Halmashauri zake zote)=173.3bln

2.Dodoma CC=53.2bln

3.Mwanza City incl. Ilemela MC=22.4bln

4.Arusha City=19.2bln

5.Mbeya City=13.0bln

6.Tanga City=12.8bln

7.Geita TC=9.2bln.

8.Morogoro MC=7.5bln

9.Kahama MC=7.12bln

10.Chalinze DC=7.1bln

11.Mkuranga DC=6.6bln

12.Mufindi DC=6.1bln

13.Moshi MC=5.7bln

14.Iringa MC=5.62bln

15.Njombe TC=5.6bln

16.Tunduma TC=5.4bln

17.Tarime DC=5.2bln

18.Kilolo DC=5.0bln

19.Mtwara MC=4.8bln

20.Mafinga TC=4.7bln

21.Tunduru DC=4.7bln

22.Muleba DC=4.61bln

23.Kilwa DC=4.6bln

24.Geita DC=4.5bln

25.Arusha DC=4.01bln.

26.Mlimba DC=4.0bln

27.Mbozi DC=3.97bln

28.Tandahimba DC=3.92bln

29.Mbarali DC=3.9bln

30.Rungwe DC=3.89bln

31.Kilosa DC=3.8bln

32.Mbeya DC=3.8bln

33.Mbinga DC=3.65bln

34.Chato DC=3.64bln

35.Kibaha TC.3.62bln

36.Chunya DC=3.5bln

My take kuna Mikoa/Miji ni ya kuonea huruma mfano Tabora,Singida,Rukwa,Katavi,Kigoma,Simiyu na Manyara.Hii mikoa haina hata Halmashauri moja yenye mapato kwa kiwango cha kuanzia bilioni 3.5 au zaidi

Kiufupi inatoa picha ya hali mbaya ya umaskini wa kipato kwa wananchi wake.Hali kadharika Mikoa ya Dar, Mbeya,Geita na Iringa ina hali nzuri ya kimapato kwa watu wake.

Pdf ya Tamisemi hii hapa [emoji116][emoji116] unaweza kujionea mwenyewe
View attachment 1763405
View attachment 1763742
Lakini yule Bwana mwenye wivu na DSM eti ni ya Wapinzani akalifuta Jiji la DSM. Mungu fundi Aliondokea zake huko huko huko kwa asiyowapenda.
 
Inakuaje Kasulu kigoma umeiacha mbona misosi na mkwanja ipo ya kutosha, ulizia wageni waliowahi kufika huku, huwa hawakumbuki kurudi tena kwao
 
Inakuaje Kasulu kigoma umeiacha mbona misosi na mkwanja ipo ya kutosha, ulizia wageni waliowahi kufika huku, huwa hawakumbuki kurudi tena kwao

Wilaya ya kasulu bado haina uwezo wa makusanyo ya bilioni 3 , ni sawa na wilaya ya masasi halafu ukumbuke kasulu wanalima mazao ya chakula hakuna mazao ya biashara ya kueleweka, ukishatoa pori la kagera mkanda kule ni pakawaida sana, maana hata mpaka wa burundi kule munanila bado haujachangamka kulinganisha na border za Tunduma na Namanga au silari, japo kuna biashara sawa na masasi
 
Inakuaje Kasulu kigoma umeiacha mbona misosi na mkwanja ipo ya kutosha, ulizia wageni waliowahi kufika huku, huwa hawakumbuki kurudi tena kwao
Kawaulize Tamisemi na DED wa huko mimi ni mjumbe tuu

Ndio hivyo haijakidhi vigezo
 
Bagamoyo imekuwaje tena? Hakuna mkwanja kivipi yaani?
1. Utalii
2. Uvuvi/Samaki
3. Kilimo
4. Viwanda
5. Ukaribu na Dar es salaam
6. Hoteli
7. Heritage site(s) - UNICEF

What is not happening???
Anatuchonganisha tu huyu!
 
Back
Top Bottom