Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Kigoma Ujiji Mc na Kyela dc wanakwama wapi wote wana maziwa makubwa ya uvuvi, wote wanalima mawese na mazao mengine ya kibiashara, wote pia wana advantage kubwa ya kuwa mpakani kabisa na nchi jirani, shida inakuwa wapi
Sina hakika kwa Ujiji, ila Kyela iko overated sana na 'wahusika'. Kabla sijafika huko nilikuwa naichukulia tofauti sn na nilivokuta uhalisia.

Wenyeji wa Kyela wanajua 'kujivimbisha' kama yule mwenzao mwenye digirii nne ila ni kawaida sana, hata mzunguko wa hela ni mdogo sana.

Hapo mpaka wa Malawi hakuna hata biashara ya maana inayofanyika ukilinganisha na mipaka mingine kama Tunduma.

Kuna wilaya kama Chunya huwezi kuisikia kiurahisi ila ina hela za madini za kumwaga, ni kamji kadogo ila mzunguko wa hela ni hatari. Kwa Chunya hizi 50m - 100m wanamiliki vijana wadogo wa kawaida kabisa lakini huwezi sikia 'mayowe'.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachaga wanajenga vijijini kwao na mikoani
Wachaga wengi wameenda shule ila nashindwa kuelewa ule ujinga wanaofanya wa kupoteza rasilimali nyingi kujenga majumba vijijini kwa ajili ya 'pride' ambayo muda mwingi wanaishi popo ukiacha zile week mbili za mwisho wa mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachaga wengi wameenda shule ila nashindwa kuelewa ule ujinga wanaofanya wa kupoteza rasilimali nyingi kujenga majumba vijijini kwa ajili ya 'pride' ambayo muda mwingi wanaishi popo ukiacha zile week mbili za mwisho wa mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafikiri kujenga kijijini sio utamaduni mbaya.
Huo umekuwa ni utamaduni wao miaka nenda rudi
 
Kutoka mjini kwenda wapi wewe mbususu..Njombe to Makambako ni km 80 hizo km 100 ni kuelekea wapi wakati unajua Mji unazungukwa na Halmashauri za Vijijini

Visingizio kibao wakati unajua fika kwamba Makambako ni kijiji kikubwa ndio kwanza kinaanza kutambaa
Hapana mkuu makambako to njome ni km59
 
Alizeti inalimwa lakini hakuna support kutoka serikalini
Kwa Singida nilicho jifunza ni kuwa, ule ulimaji wa alizeti bado ni local sana na pia msimu wa mvua ni mmoja tu kwa mwaka.

Wanaonufaika zaidi na alizeti ni wenye viwanda na walanguzi wa mazao, wakulima ambao ni kundi kubwa linaachwa hoi. Na kwa nature ya mvua za Singida, mkulima akipata mazao vizuri msimu mmoja basi unaofuatia anarudisha ile faida na pengine kuchukua na fedha zake zingine.

Kwa trend hiyo lazima mapato yawe machache kwa kuwa wenye viwanda ni wachache, tofauti na angenufaika mkulima ile pesa ingetumika kustimulate maeneo mengine kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Then unaskia sera za majimbo unabaki kujiuliza hayo majimbo yangefanya maendeleo kwa mapato gani?
Taarifa km hizi ni muhimu sana watu kua nazo kabla hawajaropoka kuhadaa uma.
Nadhani unatumia data ambazo hazipaswi kutumika kwa tathmini yako ya majimbo, na pia kwa maelezo yako inaonekana huelewi maana ya dhana ya majimbo.

Kwa haraka tu utaona haya yaliyowekwa hapa ni mapato ya halmashauri pekee, bado yapo ya serikali kuu pia. Kukiwa na majimbo (States), hizo ni serikali zinazo jitegemea kama nchi vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mkuu umeweka halmashauri yangu akati nikijicheki mfukoni kuna masalia ya maganda ya karanga tu?[emoji16] halmashauri nyingi znabebwa na uwepo wa natajiri wakubwa tu, unaweza kukuta hiyo kodi ni ya watu wachache sana.
Income inequality ni kubwa sana hapa Tz hicho sio kigezo cha kujua economic status ya mtu wa kawaida, kwa mfano mwz na dar kuna matajiri ni 1% wanao changia hiyo kodi 99% ni maxhinga mama tilie ambao ni mzingo kwa almashauri kuwahudumia hao watu......Dar na Mwz zinaongoza kwa watu wanao shindwa kupata milo mitatu kwa siku ila kimapato ndo wanaongoza.
 
Ifuatayo ni orodha ya Miji na Halmashauri 36 ambazo watu wake Wana kipato cha Uhakika na kuwa na purchasing power inayotoa fursa ya uhakika wa biashara kwa Tanzania.
Orodha imehusisha Halmashauri zenye mapato yanayoanzia shilingi za Tanzania bilioni 3.5 kwenda juu.

Orodha hii imetokana na makusanyo ya ndani ya kila Halmashauri kiutoka kwenye vyanzo vya mapato vya Halmashauri ambavyo ni shughuli za kawaida za wananchi kutoka Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mapato hayo ni nje ya vyanzo vinavyokusanywa na TRA na wakala zingine za.serikali.

Kama wewe ni mfanyabiashara hii itakuwa picha halisi ya uchaguzi wa sehemu ya kuwekeza.

1.Dar (Na Halmashauri zake zote)=173.3bln

2.Dodoma CC=53.2bln

3.Mwanza City incl. Ilemela MC=22.4bln

4.Arusha City=19.2bln

5.Mbeya City=13.0bln

6.Tanga City=12.8bln

7.Geita TC=9.2bln.

8.Morogoro MC=7.5bln

9.Kahama MC=7.12bln

10.Chalinze DC=7.1bln

11.Mkuranga DC=6.6bln

12.Mufindi DC=6.1bln

13.Moshi MC=5.7bln

14.Iringa MC=5.62bln

15.Njombe TC=5.6bln

16.Tunduma TC=5.4bln

17.Tarime DC=5.2bln

18.Kilolo DC=5.0bln

19.Mtwara MC=4.8bln

20.Mafinga TC=4.7bln

21.Tunduru DC=4.7bln

22.Muleba DC=4.61bln

23.Kilwa DC=4.6bln

24.Geita DC=4.5bln

25.Arusha DC=4.01bln.

26.Mlimba DC=4.0bln

27.Mbozi DC=3.97bln

28.Tandahimba DC=3.92bln

29.Mbarali DC=3.9bln

30.Rungwe DC=3.89bln

31.Kilosa DC=3.8bln

32.Mbeya DC=3.8bln

33.Mbinga DC=3.65bln

34.Chato DC=3.64bln

35.Kibaha TC.3.62bln

36.Chunya DC=3.5bln

My take kuna Mikoa/Miji ni ya kuonea huruma mfano Tabora,Singida,Rukwa,Katavi,Kigoma,Simiyu na Manyara.Hii mikoa haina hata Halmashauri moja yenye mapato kwa kiwango cha kuanzia bilioni 3.5 au zaidi

Kiufupi inatoa picha ya hali mbaya ya umaskini wa kipato kwa wananchi wake.Hali kadharika Mikoa ya Dar, Mbeya,Geita na Iringa ina hali nzuri ya kimapato kwa watu wake.

Pdf ya Tamisemi hii hapa [emoji116][emoji116] unaweza kujionea mwenyewe
View attachment 1763405
View attachment 1763742

Umekuja na ka-arusha kako kukasifia kwa mara nyingine, na ulivyokapamba sasa 😀 watu wa huko mnapenda sifa jamani.. eti mwanza city include na ilemela MC B22.4.. then arusha city B19.2 na arusha DC B4 😀 wasukuma sijui waliwafanya nini jamani 😀



🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
 
Nafikiri kujenga kijijini sio utamaduni mbaya.
Huo umekuwa ni utamaduni wao miaka nenda rudi
Wala sijapinga mkuu, ila ukiangalia mtu kashusha 'mansion' migombani unajiuliza kwa sababu ya nini? Tena sometimes wazee wa kichaga huwa hawapendi kuhama kwenye nyumba zao, basi ni popo tu wanajivinjari.

Nnacho jaribu kumaanisha hapa ni ile dhana ya proper use of resources, nchi ya Tanzania 'imefukia' mitaji mingi sana kwenye ujenzi wa nyumba za makazi.

Hadi mtu asiyemudu mahitaji ya kula ya kila siku unaambiwa, "usimuone vile anaishi kwake yule". Unajiuliza kama alijenga baada ya tafakari ya kina au kufata mkumbo tu.

Kujenga nyumba ya kuishi si maendeleo, katika mahitaji ya lazima (chakula, mavazi na makazi) nyumba inaangukia kwenye malazi hapo. Kwa hiyo kujenga ni kutimiza basic need si maendeleo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mwenyew nashangaa.
Hadi wilaya ya misenyi yenye viwanda kama kagera sugar,kilimo cha vanilla,mpaka wa mutukula na Ranchi kibao inazidiwa na wilaya ya muleba iliyojaa migomba na kahawa

Asilimia 80 visiwa vyote viko muleba, ushawahi kujiuliza hadi gozba iko muleba? Mapato hayo ya samaki na dagaa sio mchezo, plus kahawa ndio maana unaona viwanda kama hakika coffee wanatamba Tanzania kwa sasa na anauza pia nje ya nchi
 
Ifuatayo ni orodha ya Miji na Halmashauri 36 ambazo watu wake Wana kipato cha Uhakika na kuwa na purchasing power inayotoa fursa ya uhakika wa biashara kwa Tanzania.
Orodha imehusisha Halmashauri zenye mapato yanayoanzia shilingi za Tanzania bilioni 3.5 kwenda juu.

Orodha hii imetokana na makusanyo ya ndani ya kila Halmashauri kiutoka kwenye vyanzo vya mapato vya Halmashauri ambavyo ni shughuli za kawaida za wananchi kutoka Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mapato hayo ni nje ya vyanzo vinavyokusanywa na TRA na wakala zingine za.serikali.

Kama wewe ni mfanyabiashara hii itakuwa picha halisi ya uchaguzi wa sehemu ya kuwekeza.

1.Dar (Na Halmashauri zake zote)=173.3bln

2.Dodoma CC=53.2bln

3.Mwanza City incl. Ilemela MC=22.4bln

4.Arusha City=19.2bln

5.Mbeya City=13.0bln

6.Tanga City=12.8bln

7.Geita TC=9.2bln.

8.Morogoro MC=7.5bln

9.Kahama MC=7.12bln

10.Chalinze DC=7.1bln

11.Mkuranga DC=6.6bln

12.Mufindi DC=6.1bln

13.Moshi MC=5.7bln

14.Iringa MC=5.62bln

15.Njombe TC=5.6bln

16.Tunduma TC=5.4bln

17.Tarime DC=5.2bln

18.Kilolo DC=5.0bln

19.Mtwara MC=4.8bln

20.Mafinga TC=4.7bln

21.Tunduru DC=4.7bln

22.Muleba DC=4.61bln

23.Kilwa DC=4.6bln

24.Geita DC=4.5bln

25.Arusha DC=4.01bln.

26.Mlimba DC=4.0bln

27.Mbozi DC=3.97bln

28.Tandahimba DC=3.92bln

29.Mbarali DC=3.9bln

30.Rungwe DC=3.89bln

31.Kilosa DC=3.8bln

32.Mbeya DC=3.8bln

33.Mbinga DC=3.65bln

34.Chato DC=3.64bln

35.Kibaha TC.3.62bln

36.Chunya DC=3.5bln

My take kuna Mikoa/Miji ni ya kuonea huruma mfano Tabora,Singida,Rukwa,Katavi,Kigoma,Simiyu na Manyara.Hii mikoa haina hata Halmashauri moja yenye mapato kwa kiwango cha kuanzia bilioni 3.5 au zaidi

Kiufupi inatoa picha ya hali mbaya ya umaskini wa kipato kwa wananchi wake.Hali kadharika Mikoa ya Dar, Mbeya,Geita na Iringa ina hali nzuri ya kimapato kwa watu wake.

Pdf ya Tamisemi hii hapa [emoji116][emoji116] unaweza kujionea mwenyewe
View attachment 1763405
View attachment 1763742
Hii haihusiani na ubora wa maisha katika halmashauri hizo, wala kipato cha mtu binafsi katika halmashauri husika. Kuna halmashauri zenye mapato makubwa kwasababu kuna mradi mmoja mkubwa pale. Mfano Mlimba kuna mashamba ya walowezi ya mitiki, ni makubwa na ndio chanzo kikubwa cha kodi. lakini kipato binafsi na hali ya maishi iko chini mno!
 
Umekuja na ka-arusha kako kukasifia kwa mara nyingine, na ulivyokapamba sasa [emoji3] watu wa huko mnapenda sifa jamani.. eti mwanza city include na ilemela MC B22.4.. then arusha city B19.2 na arusha DC B4 [emoji3] wasukuma sijui waliwafanya nini jamani [emoji3]



[emoji1033][emoji1033][emoji1033][emoji91][emoji91]
Takwimu zimetoka Tamisemi sijatunga mimi.

Afu mada haijaanzishwa kwa mantiki unayowaza wewe,unaonesha una infiriority complex
 
Back
Top Bottom