Eeh bwana, kama saa hizi hakufai kabisa, kuna baridi na mvua za ajabu ajabu tu japo ndiyo zinaishia. Ila yote tisa kama unataka kuwekeza kwa muda mrefu, Mufindi is the best place. Ardhi inapatikana kirahisi kwa gharama nzuri. Vibarua wapo wa kutosha tena waaminifu sana: Zao ambalo linalipa kwa muda mrefu kama una mtaji wa kutosha ni miti na parachichi.
Ukipanda parachichi ukanda huu, huwa zinazaa kipindi cha tofauti na sehemu nyingine, hivyo wakati hayapatikana kwa urahisi sehemu nyingine huku ndiyo yanaanza kutoka. Karibu sana Mkuu, naamini mambo yatakaa poa tu, Mama kasema atakuwa hatunyang'anyi pesa zetu na kutubambikizia kodi kama Marehemu alivyokuwa anafanya.
PEACE OUT [emoji3577] [emoji3577] [emoji3577] [emoji3577]