Hii ndio sababu kwanini familia ( ndugu walio zaliwa tumbo moja)nyingi sasa hivi zimeparaganyika

Hii ndio sababu kwanini familia ( ndugu walio zaliwa tumbo moja)nyingi sasa hivi zimeparaganyika

Usasa katika makuzi na kuthamini kipawa cha kila mtoto na kuacha kumbeza mmoja huku ukimsifu mwingine! Kumchukia mmoja na kumpenda mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Najifunza.

Mimi nilikuwa nadhani ni kwenye familia yetu tu ila kupitiq comment za watu huko insta nikagundua kumbe ni jambo la kitaifa
 
Wazazi ni chanzo cha kuparanganyika , kupendelea watoto wenye uwezo fulani ,zaidi ya wengne bila kujua kila mtu ana umuhimu wake ,hii ni sumu mbaya sna ya utengano kati ya ndugu wa damu.
 
Mfumo wa maisha kwa sasa umekuwa mgumu sana, hela imekuwa ndio muamuzi wa mambo mengi na jamii nyingi zimevurugwa na utafutaji.

Famili nyingi za kirofa aka kimasikini ndio zimeparaganyika maana wengi hawana kipato cha kuwakutanisha kwenye matukio kama misiba, harusi na hata mikutano ya kifamilia.

Familia nyingi za kitajiri zina wasaa wa kukutana kwenye matukio yanayounganisha familia hata kuwa na vikao vya kuamua mustakabali wa mambo mengi ya kimaisha ndani ya familia.

Wazazi wakiwa hai kushindwa kutengeneza familia bond hasa kuitisha vikao vya mara kwa mara na kukutanisha ndugu mbalimbali hata kutembelea nyakati za weekend na kuchoma mbuzi familia A na familia B.
 
Nimekutana na ujumbe huu instagram na kila mtu Anasema unamgusa.

" Ukweli ni kwamba familia nyingi zimeparaganyika SASA hivi kwa sababu walio kuwa wanaziunganisha( wazazi) wamekwisha tangulia mbele za haki"

Wazazi wetu waliweza vipi kuunganisha familia hata sisi wa kizazi huko tushindwe?


Mohamed Said

Nguruvi3

Kiranga

Mshana Jr

digba sowey
Inategemea wazazi wakiondoka kma upendo wao upo
 
Asante kwa mwaliko,Ni kweli usemacho bwana LIKUD ila mimi nadhani malezi yanayotolewa na wazazi ambayo unakuta yameegemea upande mmoja ndiyo chanzo kikubwa katika kuparaganyika kwa familia baada ya wao (wazazi)kuondoka duniani,bila kuficha mfano hapa jirani yangu Kuna familia ya watoto nane ,baba wa familia alishatangulia mbele za haki ,kabaki mama pekee,hawa watoto wa hii familia hawaishi kurumbana kila wakutanapo na hasa Kuna vijana wawili ambao ni jobless ambao wanatuhumiwa kupendelewa na mama yao mzazi na Mara nyingi hufuja Mali za nyumbani bila mama yao kutoa onyo,hali hii imepelekea watoto wale sita wahisi kuwa mama yao ana malezi yanayo lalia upande mmoja,hivi unadhani baada ya mama yao kufariki watoto hawa watakuwa na umoja tena au ndo kusambaratika kwa familia!!?


Hivyo nihitimishe kuwa malezi mabaya ya wazazi ambayo watoto wengi huhisi kuwa yamegemea upande mmoja ndiyo chanzo kikubwa cha uzao kuparaganyika baada ya wazazi kuondoka hapa duniani,nashauri sisi wazazi wa Leo tuwe umakini sana katika malez yetu ambayo yatafanya vijana au watoto wetu waamini kuwa wako level moja kwa wazazi wao
 
Back
Top Bottom