Mfumo wa maisha kwa sasa umekuwa mgumu sana, hela imekuwa ndio muamuzi wa mambo mengi na jamii nyingi zimevurugwa na utafutaji.
Famili nyingi za kirofa aka kimasikini ndio zimeparaganyika maana wengi hawana kipato cha kuwakutanisha kwenye matukio kama misiba, harusi na hata mikutano ya kifamilia.
Familia nyingi za kitajiri zina wasaa wa kukutana kwenye matukio yanayounganisha familia hata kuwa na vikao vya kuamua mustakabali wa mambo mengi ya kimaisha ndani ya familia.
Wazazi wakiwa hai kushindwa kutengeneza familia bond hasa kuitisha vikao vya mara kwa mara na kukutanisha ndugu mbalimbali hata kutembelea nyakati za weekend na kuchoma mbuzi familia A na familia B.