Hii ndio sababu Magenius hawawezi kuwa matapeli

Hii ndio sababu Magenius hawawezi kuwa matapeli

Duniani tumo binadamu wa aina tatu kiakili na wote tunaishi pamoja in harmony na tumegawanyika katika makundi makuu matatu kiutendaji na utekelezaji wa akili zetu.

Kundi la kwanza ni wale Magenius.. Hawa mabwana wana IQ kubwa kuliko binadamu wa kawaida wana score around (160 - 300) wana uwezo mkubwa sana wa kuchakata taarifa vichwani mwao na kufumbua mafumbo magumu kuliko ila bahati mbaya zaidi hawa asilimia 90% yao ni wagonjwa wa ugonjwa wa usonji( Autism). Ugonjwa wa akili huu, ugonjwa huu wa usonji mara nyingi huwapata wakiwa watoto wa mwaka na nusu na kuendelea. Dalili zao huwa wanapenda kukaa peke yao, hawapendi kelele, wanachelewa kuongea, wana hisia Kali sana za kunusa na kusikia na wako very bright kwenye kitu kimoja pekee. Na pia huwa wanaongea kidogo sana..they only do "small talk" they are not good conversationalist. Sio waongeaji wazuri sana.

Nilifuatilia zaidi na kuyajua mengi juu ya Autism baada ya mpwa wangu kugundulika ana ugonjwa huu wa usonji akiwa na miaka 3..huyu dogo ana miaka 10 tu kwa sasa mnaweza kuwa mmekaa nje akawambia mtoto analia na kweli after a second dogo analia ndani...then mmekaa nje anakwambia maharage yanaungua..na kweli mnasikia harufu ya maharahe kuungua jikoni punde baada ya yeye kusema. Wako very sensitive. Ni wakimya na pia very loner..wanapenda kukaa wenyewe tu na huwa wanaconcetrates na kitu kimoja tu mawazoni mwao huyu dogo shuleni ni mtupu but he is very artistic genius and creative, unaweza ukatembea nae mjini then mkirudi home anadrawing kit yake ya kuchorea tu anachora mji mzima mlimopita kwa usahihi bila kurejea popote pale hadi huwa navurugwa ufahamu ukizingatia Mimi hata kuchora kagari tu siwezi. Nikagundua dogo is genius sababu ya ugonjwa wake wa usonji.

Nikarejea historia ya Michelangelo na Vincent Von Gosh hawa wote walikuwa artistic genius..huyu Van Gosh alikuwa anaweza kuuchora hadi upepo unaovuma..hakyamungu! This is insanely genius..ukingalia kwenye picha zake za starry starry night utaona kazi zake but alikuwa mwehu na michoro hii aliichora akiwa kwenye chumba cha vichaa alipojipiga risasi na kufariki akiwa mpweke sana. Michaelangelo huyu ni balaa yeye hata simzungumzii maana anahitaji Uzi wake kabisa ili tumtendee haki. Tukipata muda tutamjadili.

Albert Einstein Mwanamahesabu na mwanafikizia ambae amebadilisha maisha ya binadamu anaaminika kuwa the most influential scientist of the 20th century, amechangia mengi kwenye aerospace engineering, astrophysics, mathematic, spirituality e.t.c alifanya kazi kubwa ya sisi kuishi hivi Leo kwa theory yake of relativity ya E=MC sqaure ndio theory iliofagia njia ya kutengeneza mabomu ya nyuklia Leo hii. Akiwa na miaka 10 usonji ukiwa umemuandama hakuweza kuongea vizuri wala kuwa na marafiki akiwa na IQ kubwa kabisa aliweza kufaulu somo moja tu la hisabati tu shuleni yaliyobaki alifeli vibaya sana. Alipofikisha miaka 16 alikuwa anaitwa chuoni kusolve complex mathematics equations zilizowashinda maproffesor na akiwa na miaka 25 hakukubaliwa na vyuo vingi maana kwenye mtihani wa kujiunga na chuo alifaulu somo moja pekee mathematics kwa asilimia 100. Watu hawa huwa wanakuwa na ugonjwa wa Usonji unaowafanya kufikiri kitu kimoja tu deeply kutokana na nerve circuit zao zilivyoundwa kwenye brain. Magenius maarufu Waliothibitika kuwa na Autism ni Albert Einstein, Charles Darwin, Sir Issac Newton, Michelangelo, Aristotle, Tesla e.t.c Wengi wao wana muandiko mbaya sana maana mikono yao haiwawezi kuendana na kasi ya ubongo unavyofikiri, hivyo wanajikuta wanaandika fasta na rough ili kukimbizana na kasi ya ubongo wao unachokifikiria.

Tunahitimisha kwa kukubaliana na mwanafalsa maarufu wa ugiriki ya kale kwamba any genius is accompanied with some sense of madness.. Magenius wengi ni vichaa na hii inapigiliwa msumari na kauli hii "too much of anything is harmful " akili ikizidi kipimo muhusika anakuwa hayuko normal na hivyo anakuwa psychiatric Case hivyo ni ngumu sana kichaa kukutapeli maana ni mgonjwa wa akili maana ana complex things kichwani ambazo hata yeye hawezi na hana lugha ya kuzielezea kwa watu wakamwelewa kirahisi atawezaje kukushawishi uingie mkenge!? Jibu ni hawezi kukutapeli maana hata hawana good socializing ability kama wengine. lakini hapa sasa ndipo linapoibuka kundi la watu wengine wanaitwa "intelligent people" watu hatari sana hawa.

Hawa intelligent people bongo zao ziko katikakati kiakili wana uwezo wa kupata maneno sahihi ya kuelezea zile complex ides za genius..hawa uandika hata zile manual zinavoelezea namna ya kutumia vitu mbalimbali vilivyoundwa na magenius kwa lugha rahisi na nyepesi maana wanayo maneno sahihi na ya kueleweka kirahisi, hawa wanaandika kimkakati hoja zao na kuweza kushawishi watu kirahisi sana kama alivyosema Fid Q msanii wa hip hop kwamba "neno zuri huwa halina ukweli na neno baya ndio lenye ukweli " hawa intelligents siku zote Daima dumu wana maneno sahihi na matamu ya kukufanya uuone ukweli au usiuone.. Aina ya watu hawa ni Adolph Hitler, Barack Obama, Hemingway, e.t.c na Kwenye hili kundi wanakaa matapeli pia Kariba ya brother wa Forex n.k sijawahi kuona katika maisha yangu tapeli asie jua kupachika maneno sahihi na matamu kwenye maandishi au maneno yake. Sijawahi kumuona! Mtaji wao ni maneno yake matamu.

Then group la mwisho ni "normal people" au tunafahamika zaidi kama watapeliwa Ahahaha. Sisi tunafit Kwenye social world maana tunaenda clockwise na jamii yetu na bongo zetu hazijisumbui kuchakata taarifa zaidi wala kuconcertrates na kitu kimoja we are carefree hatuna tofauti na simu za Motorola za zamani mwanga ukizima zinazima moja kwa moja hadi ndani tofauti na intelligents ambao wao ni simu janja(smartphone) zenyewe screen ikizima na kuwa nyeusi ujue imezima kinafiki internal background inaprocess more informations kifupi hazilali bongo zao tofauti na normal people sisi ambao ni kundi kubwa akili zetu ni za kawaida sana na ndio akili za binadamu wenye afya na wazima kiakili maana hatuoverload brain zetu na sisi sio wagonjwa wa akili kama hao wawili hapo juu wanaosumbukiwa na Autism na Bipolar disorder.

Tujitahidi tujue mechanism za matapeli na tuwaepuke mapema before its too late.

Na je unadhani wewe unafit group gani hapo juu? Kwanini unahisi group ulilochagua linakufaa? Tupe sababu?
ndeefu lakini tamuu.
 
Ubongo wenye ugonjwa na ule mzima usioumwa ni upi una afya na wenye kufanya kazi vizuri?
 
Mtu yeyote mwenye uwezo wa kuchora, anakua na akili sana.
Pia kundi la Intelligents, wanapenda ni hatari kwa nkupiga kazi (sijui kwa wanawake, hapa narejea wanaume). Majinias wenyewe hawana muda na hayo mambo.
 
Hivi Karibuni kumeibuka mjadala mkubwa sana huko majuu baada ya maprofesa kugawanyika kuhusu Kanye West kwamba ni genius au ni mwehu kutokana na vitu anavyovifanya na kuviongea..aliwaambia watu wachague nyimbo mbaya zaidi Duniani na atazigeuza kuwa nyimbo za kuuza album yake..watu wakachagua ngoma tatu then akazifanyia uchawi wake zikawa ndo best kwmeye album yake ya famous.

Mbali na hayo kuna vitu anavisema vinaashiria jamaa yuko ahead of our time. Yaani anaishi future.

Kanye magharibi au kanye West.

Hii ya Kanye West iko subjective kwasababu inaondoa ukweli kuwa umaarufu pekee huufanya mwimbo kuwa bora. Wafuasi wa Kanye watatafuta visababu lukuki ili waupende mwimbo wake hata kama si mzuri.
 
Hii ya Kanyewest in very subjective kwasababu inaondoa ukweli kuwa umaarufu pekee hufanya mwimbo kuwa bora.
Achana na hiyo ya wimbo though kuna hundred of artist wamejaribu kufanya kama anachofanya kanye na hizo old songs but they have failed miserably.

Kuna vitu kibao anaongea inaonyesha kabisa the muhufuka is living our future.

Kuna professor mmoja amemfanya kama case study anamsoma kanye tu practically.
 
I'm introvert
na nipo group la kwanza yani sifa zote ulizoandika ni kama unanizungumzia Mimi ,napenda sana hesabu nimeanza kuipenda tangu shule ya msingi hadi sasa nipo chuo na ndo somo ambalo nimefahuru kuliko mengine na natamani ningekuwa nasoma hesabu tu,pia unavyomzungumia Albert Einstein's kuhusu kumudu hesabu kuliko masomo mengine kipindi Yupo chuo ni kama Mimi tu nilivyo,
pia napenda sana kujifunza vitu vipya vyipa muda wote kupita kusoma yani najikuta nasoma kila aina ya takataka sijali inahusu business, gambling,science,
pia napenda sana kusikiliza music ,kucheck movies sipendi,napenda muda mwingi kukaa peke yangu,pia muda wote nafikiria sana vitu vingi vingi ,
wakati nipo semester ya kwanza nilijishangaa sana ,na pia wanafunzi wenzangu walishangaa sana baada ya kupata 100% business mathematics

Ni kweli unavielemea vya akili nyingi na hiyo kupenda kusoma na kufikiri ni asset kubwa sana katika dunia ya sasa.

Siku hizi processing and interpreting data ni tatizo kubwa sana duniani, kuna data lukuki lakini watu wanaoweza kuzielezea na kuzitumia ipasavyo ni wachache sana.

Watu kama nyinyi ndiyo mtahitajika sana huko mbeleni na hasa kama unajua ku code algorithms (unaweza fika mbali sana). Na weza ku suggest usome kitabu kinaitwa "Automate this" cha Christopher Steine kinaelezea jinsi algorithms zinavyoendesha dunia hii ya sasa.
 
Sawa mkuu, lakini uzuri ni kwamba, ukikutana na mmoja kwenye eneo lake haitachukua muda kumtambua.

True that.

But are those so called geniuses know it all or?

Manake unaweza kukuta mtu anaitwa genius kisa tu anajua ku solve math problems lakini hajui hata kupigilia msumari kwenye mbao za kitanda!

It’s far more complicated.
 
Tunahitimisha kwa kukubaliana na mwanafalsa maarufu wa ugiriki ya kale kwamba any genius is accompanied with some sense of madness.. Magenius wengi ni vichaa na hii inapigiliwa msumari na kauli hii "too much of anything is harmful " akili ikizidi kipimo muhusika anakuwa hayuko normal na hivyo anakuwa psychiatric Case hivyo ni ngumu sana kichaa kukutapeli maana ni mgonjwa wa akili maana ana complex things kichwani ambazo hata yeye hawezi na hana lugha ya kuzielezea kwa watu wakamwelewa kirahisi

kushindwa kumuelewa mtu hakumfanyi muhusika kuwa kichaa. Hivi mtu akihoji kuwa psychiatry hana chembe ya uwezo kiakili kumkaribia huyo genius ndiyo maana hamuelewi, utamjibuje?

atawezaje kukushawishi uingie mkenge!? Jibu ni hawezi kukutapeli maana hata hawana good socializing ability kama wengine. lakini hapa sasa ndipo linapoibuka kundi la watu wengine wanaitwa "intelligent people" watu hatari sana hawa.

Humble African said:
Kwa hiyo genius ni wehu hawana ufundi wa kutapeli kama intelligent wao ni naturally matapeli...professional zao ni siasa au conmen.

Usijali..utaelewa taratibu tu.

Hivi kushindwa kutapeli watu ni wehu?

kama mtu haoni umuhimu wa kutapeli wengine kwasababu anaona kufanya hivyo ni kutokuitendea haki akili yake, kwa kuwa yeye anajali zaidi kuitumia kutatua mambo makubwa zaidi kwa jamii, huoni kuwa hapa kuna utofauti wa kimtazamo zaidi ya uchizi?
 
Achana na hiyo ya wimbo though kuna hundred of artist wamejaribu kufanya kama anachofanya kanye na hizo old songs but they have failed miserably.

Kuna vitu kibao anaongea inaonyesha kabisa the muhufuka is living our future.

Kuna professor mmoja amemfanya kama case study anamsoma kanye tu practically.
Ni vitu gani anavyoongea Kanye ambavyo mwenzetu unaviona vina akili?
 
True that.

But are those so called geniuses know it all or?

Manake unaweza kukuta mtu anaitwa genius kisa tu anajua ku solve math problems lakini hajui hata kupigilia msumari kwenye mbao za kitanda!

It’s far more complicated.

Kwanza, nakubaliana na wewe kwamba kimsingi, kwamba tunaouita u genius ni mada pana sana na hapa tumeigusa kwa juu juu kutoa mwanga kwa mujibu wa mleta mada.

Tukirejea alichoandika Humble African , ametolea mfano walioitwa magenius wachache kwamba walijikita kwenye eneo moja. Mwingine Physics, wengine Chemistry au mahesabu. Hawa hawakuishia kuelewa au kukokotoa mahesabu tu bali walienda mbali zaidi kwa kugundua namna hayo masomo yanavyoweza kutusaidia kwenye maisha ya kawaida. Sasa kwa wale ambao ni wazuri kwenye somo kwa maana ya kukokotoa au kuelewa na kumudu somo moja bila kwenda mbali zaidi namna ya kuutumia huo uwezo nao tuwaite magenius?

Hapohapo linaibuka duala la vipaji, kuna watu wanacheza mpira hatari, au wanaimba kuliko mfano, au wanakumbukumbu isiyo kawaida na wengine wachoraji wa kutisha, hao nao ni ma genius kwenye maeneo yao?

Sijaelewa pia unaposema hawawezi KUTAPELI, kwanza itafsiriwe maana ya utapeli. Kuna yule mfaransa kama sikosei aliitwa Carlos tukapata habari zake nyingi sana za uhalifu. Huyo tunamuweka wapi? Nnachofahamu michongo na mikakati mingi iwe ya utapeli au yenye tija inahitaji kiwango cha juu sana cha akili.

Mwisho, ni utahira au ukichaa kiasi gani unahisishwa na hao wanaoitwa ma genius?
Na je, inawezekana tunaowaona vichaa wakawa na chembechembe zozote za u genius (nafikiri kuna haja ya utafiti kufanyika).

Kwa muktadha huo, huu ni mjadala mpana japo hii post imetupa mwanga.

Shukrani mkuu
 
Back
Top Bottom