Hii ndio Sababu ya Mungu Kutoonekana

Hii ndio Sababu ya Mungu Kutoonekana

FabNXTzqEtcgazfbjjfo

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
1,486
Reaction score
1,874
Mwenye Enzi Mungu haonekani kwa Sababu yeye hayupo pamoja na Viumbe wake. Yeye yupo alipo na Viumbe wake wapo walipo hana Upendeleo na Kiumbe Yeyote yule bali ana Enzi na Viumbe wake

Yeye hausiani na Viumbe wake na Wala hakai na Viumbe wake aliwaumba na Kuwaweka Katika Sayari zake na Kila Kiumbe akamjalia akili za Kuishi kwake

Habari za kwamba Mwenye Enzi Mungu Anaongea na Viumbe wake kupitia Malaika au Mwenyewe alikuwepo Duniani si Habari Sahihi. Na kama Ingekuwa hivyo mpaka leo hii basi Angekuwa anakuja Na Kuongea na Viumbe wake

Maana Kulingana na Vitabu Mwanzo alikuwa Anaongea na Kutembea bustanini na Kuongea na Viumbe wake ila Baadae akaacha na Kuanza kutuma malaika. Ila leo hii Hata hao Malaika Hawaonekani tena, Dhana hii Haiingii akilini Kwa Mtu anayetumia akili Timamu. Kitu kinachopelekea kwamba watu wengi wamepotoshwa kumhusu Mungu na Viumbe waovu.

Mwenye Enzi Mungu hakuwahi kufanya hayo yote hajawahi kaa na Viumbe wake wala kutuma Viumbe waende kwa Viumbe wengine kumuelezea yeye alivyo.

Hawa wanaoleta Ujumbe na Kusema Ni Ujumbe wa Mungu hawajatumwa Na Mungu mwenye Vyote bali ni Viumbe waharibifu waliokuja Duniani kimagendo. Na kuwaingia watu na Kusema Kupitia Vinywa vya Watu. Kama Vile Jini anavyoingia Kwa Mtu na kusema atakavyo.

Mungu Haonekani kwa Sababu hakai na wewe hapa Duniani na Hawezi onekana a maana Hayupo pamoja na Viumbe wake. Yeye yupo alipo na Wewe upo alipotaka uwepo

ASANTENI
 
Mwenye Enzi Mungu haonekani kwa Sababu yeye hayupo pamoja na Viumbe wake. Yeye yupo alipo na Viumbe wake wapo walipo hana Upendeleo na Kiumbe Yeyote yule bali ana Enzi na Viumbe wake

Kwahiyo unachomaanisha tukisali hatusikii na wala hatuoni??!!! Kwamba yeye yupo huko aliko,,na sisi tu huku tulipo ni kama umemaanisha ametutenga au nimekuelewa vibaya mkuu??!
 
Mleta mada ndezi kweli wewe, hao majini uliowaongelea walitoka kwa nani kama sio kwa Mungu? Walikuwa ni malaika waliomwasi Mungu.

Kwa taarifa yako Mungu yupo na viumbe vyake na yupo mahali pote, na malaika zake wema wapo kila mahali, ndo maana hayo majini uloyasema yakipigwa kwa neno la Mungu na Malaika zake kupitia watumishi wake yanalipuka na kukimbia.
 
Ndugu Mtafiti kuhusu Mungu, kuna wimbo Afande Sele alisema;
"....ndio maana Bwana Mungu amejificha haonekani, anaogopa lawama/ na watu wenye shida kumuandama/"
Weka neno ndugu mtafiti.
Mungu akuogope wewe ili iweje wakati kakuumba. Anaogopaje lawama kwa Kiumbe wake

Mungu si Muoga na Wala hana Sifa hizo mnazompa. Mwoga na Mwenye lawama ni Wewe na Mimi.

Shida Ni matokeo ndio maana Wengine wanazo na wengine hawana
 
Kwahiyo unachomaanisha tukisali hatusikii na wala hatuoni??!!! Kwamba yeye yupo huko aliko,,na sisi tu huku tulipo ni kama umemaanisha ametutenga au nimekuelewa vibaya mkuu??!
Toa kwanza Imani ulizoambukizwa kuhusu Mungu ndipo utaelewa. Nimeshasema Mungu hakai na Viumbe wake Unaposema amekutenga inamaana wewe ni kiumbe Wake wa Pekee kuliko majini.. Malaika n.k

Keshakupa akili ya kuishi na Kujua Ukweli
 
... malaika ni viumbe au sio viumbe?
 
mleta mada ndezi kweli wewe, hao majini uliowaongelea walitoka kwa nani kama sio kwa Mungu? Walikuwa ni malaika waliomwasi Mungu.

Tumia tu Akili Timamu ndugu yangu. Malaika na Majini wana uhusiano gani malaika ni kiumbe kingine na Jini ni Kiumbe kingine

Kwa taarifa yako Mungu yupo na viumbe vyake na yupo mahali pote,

Kwahiyo Unaposema yupo na viumbe vyake mana Yupo hata Kwenye makazi ya Shetani na Majini. Na Unaposema yupo mahali pote inamaana Hata Chooni/Mfukoni mwako yupo ndugu yangu.

na malaika zake wema wapo kila mahali, ndo maana hayo majini uloyasema yakipigwa kwa neno la Mungu na Malaika zake kupitia watumishi wake yanalipuka na kukimbia.

Umekaririshwa tu Ndugu yangu ndio maana Unaongea hivyo. Hujui kuna Malaika waovu na Washenzi. Unaposema malaika wanatumwa na Mungu kupigana na Majini na Yanakimbia

Kwenye hivyo hivyo vitabu Malaika walikuwa wanatumwa na Kupigana na hao viumbe na Wanashindwa. Sasa ushajiuliza Mungu anaweza Tuma Kitu halafu kikashindwa. Refer Biblia yako utaona jinsi gani Malaika walivyokuwa wanashindwa vita waliotumwa na Mungu kwenda kupigana

Ndio ujue Kwamba hizo Vita ni za Viumbe kwa Viumbe siyo vita za Mungu
 
Kwahiyo unachomaanisha tukisali hatusikii na wala hatuoni??!!! Kwamba yeye yupo huko aliko,,na sisi tu huku tulipo ni kama umemaanisha ametutenga au nimekuelewa vibaya mkuu??!
Mungu kaacha Muujiza wake. Unaotenda kazi.

Usimpe sifa ya Kusikia na Kuona maana Vinavyosikia ni masikio na Macho ndio yanaona hivyo vitu unavyowewe Binadamu kwenye Mwili Wako
 
Back
Top Bottom