Hii ndio Sababu ya Mungu Kutoonekana

Ukweli unaujua Ila unajitoa akili yaani unajifanya hamnazo
Hii ni Forum huru. Si kila unachokijua wewe ndio ukweli. Unaweza Ukawa Umepotoshwa pia ndio mana unajaa Hasira

Fuatilia kitabu Ulichonacho utajua kwamba Mambo mengi yaliyoandikwa si Mambo ya Mungu bali viumbe walikaa wakaandika yao ili wakupotoshe akili yako na Watawale Hii dunia watakavyo.

Fuatilia kwa Makini utajua kwamba kuna Vita vilipoganwa kwenye hivyo vitabu vinaonyesha wazi kwamba malaika wa Mungu walipigwa na Wakashindwa na Shetani. Sasa Mungu anatumaje Malaika halafu wakaenda Kupigwa na Kushindwa
 
nafikiri mada yako ingekuwa na mashiko kama ungelizia kuwa; HAYO NI MAWAZO YAKO!
Namaanishe usitake kuaminisha watu waamini unachokiamini kwani kila mtu ana uhuru wa kufikiri na kuja na mawazo yake!
Mawazo yangu kuwa Tofauti na Yako haimaanishi wewe usitumie Akili timamu Kujua Ukweli au Uongo.

Sijataka Uamini nimetaka wewe utumie Akili Timamu kujua Mambo kuamini na Kutoamini si Jukumu langu hilo ni Lako mwenyewe. Hata Hizo dini mlizoletewa Ziliwakuta Mna Imani Zenu ila Mkazipuuza Mkaamini Hizo na Mpaka leo mnazitetea bila Kujua Ukweli
 
Ile miujiza ya uponyaji inakujaje?
Nahitaji kujua
Uponyaji upo ila Si Kwa Miujiza hiyo unayoiona kwa Sasa Watu hawaponywi wanapata Nafuu.

Ndugu yangu Hospitali zikiwa nyingi unachotegemea ni Wagonjwa Kupungua Si kuongezeka. Sasa hivi makanisa ya Uponyaji wa kimiujiza yanaongezeka na Wagonjwa wanazidi ongezeka. Wengi hutoa shuhuda za uongo Kuaminisha watu ili makanisa yajae

Ndugu yangu Miujiza unayoiona Mingi si miujiza ya Mungu mwenye Vyote maana hata Wachawi na Waganga pia wana Miujiza
 
Sasa wale wa kwa ma nabii na mitume wanaosema wamemwona huwa wanaona nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa.uponyaji genuine unakujaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…