Labda tukupe somo kidogo kuhusu upangaji wa timu kwenye hatua ya makundi..
Timu zilizoingia makundi ni kumi na sita (16) ambazo zinapangwa kwenye poti nne tofauti kutokana na ranks ilizonazo kwenye msimamo wa timu bora Caf,Sasa ukiangalia hapo Yanga ipo poti namba mbili(2) kwa maana hiyo sasa watakapo panga makundi kutakua na makundi manne yenye timu nne nne,Hivyo basi kila timu iliyopo kwenye poti husika itakutana na timu moja moja kutoka kwenye mapoti mengine yani mfano timu ipo kwenye poti namba mbili ni lazima ikutane na timu moja kutoka poti namba moja,kutoka poti namba tatu na pia kutoka poti namba nne..
Hapo ndio itakua imekamilisha idadi ya timu nne kila kundi..Sasa ukiangalia hapo Yanga ipo poti namba mbili manake Yanga ni bora ukilinganisha na timu zinazopatikana poti namba tatu na nne hizo ndio timu zinazotakiwa kumuhofia Yanga na sio Yanga kuwahofia wao,Yanga timu inazoweza kuzihofia ni timu zinazopatikana poti namba moja tu na zenyewe ni timu moja tu ndio itakua kundi moja na Yanga..
Na kati ya hizo timu zinazopatikana kwenye poti namba moja ni moja tu ambayo Yanga haijakutana nayo kwenye mashindano ya Caf kwa misimu hii mitatu lakini zingine zote zimeshakutana na Yanga.