Hii ndio siri ya wasukuma kuhusu utoaji wa zawadi kubwa kwenye send-off zao

Actually sio wasukuma, makabila mengi sana wamechukulia sherehe/ndoa ni sehemu ya kupiga pesa za wanamichango.

Ni nadra sana kuona harusi za mwanaume anayefunga ndoa, wazazi wake wanawapa zawadi ya million 200, 100 n.k mara nyingi harusi nyingi zinazotrend zawadi nyingi Huwa ni send-off tu, mara nyingi comment unaziziona kutoka Kwa watu Huwa wanasema ""bwana harusi ajipange"

Kile unachokiona kwenye send off zoote Huwa ni kiini macho, ni utapeli mtupu ndio maana harusi iliyofanyika juzi katoro zawadi ilivyotajwa billion 1, bibi harusi hakuonyesha reaction yoyote, kwasababu alikua anajua sio za kwake.

Wazazi wanaandaa sherehe ya gharama na kuita watu wengi, lengo ni kukusanya pesa nyingi na zawadi ya kwenye kamati huwa hapatiwi bibi harusi ila familia/baba ndio anabaki na hiyo hela, bibi harusi anabaki Hana Kila kitu familia inajilipa hizo pesa za zawadi.

Mshikaji wangu mwaka jana alioa, kwenye send off ya MKE wake alikuepo akasikia zawadi ya kamati ni million 17 akasema maisha si ndio aya? Baada ya harusi anamuuliza Mke wake vipi kuhusu pesa maana anashangaa kuona masufuria tu lakini pesa hazioni, MKE wake akamwambia pesa kabaki nazo baba.

Yaani umelipa mahari laki 8 alafu kirahisi tu MKE wako azawadiwe billion 1 aje nazo kwako?

Mwaka huu Kuna mfanyabiashara alikaribia kufirisika kwenye mitikasi yake hapo mwanza, akaona michongo aieleweki akafanya sherehe kubwa Kwa shemeji yake (Kwa kisingizio cha kwamba amemlea yeye) kukusanya watu wengi, zawadi ya kamati million 24 jamaa ikamboost kurudi mjini.

Msitishike na hizo sherehe hapo bibi harusi anaondoka na vyombo tu.

Hakuna
Mimi ni mwana kanda ya ziwa, uliyoyasema yana ukweli kwa asilimia kadhaa(KUTOKANA NA FAMILIA UTAKAYOOA)

Mimi nilioa mwaka fulani, mke wangu alifanyiwa sendoff kwao....pia ni fundi nguo....

Alichokuja nacho ni vyombo tu! Hata cherehani aliyokuwa anashonea(ya kwake) alikatazwa asije nayo KWAMBA MME WAKO ATAKUNUNULIA!

Hela ya zawadi ya kweli, NI HELA YA HARUSI INAYOFANYWA NA MME!

Pia mkumbuke huwa KUNA KUONGEZA SIFURI (Mfano kwangu niliwapanga Mama,Dingi mdogo mmoja na Mjomba mmoja Na kuwapa hela niliyoazima kwa mtu...

kila mtu nilimpa mil 1 atoe zawadi(HII HUFANYWA SANA HUKU ILI KUVUTA WATU WATOE ZAWADI YAANI WAKUUNGE)

ukisema utoe laki utaungwa ef 5 tano tu...

Nna real experience kwangu mwenyewe...(I can assure you hiyo bil 1 iliyotolewa binti anaweza kupewa mil 50 tu akaanzie maisha) nna uhakika na hilo...Usinibishie!

Pesa yoyote upande wa mke, mwanaume huna mamlaka nayo! Wala huwezi kuihoji!
 
Watu wenye uwezo mkubwa wapo kibao , siku hizi hakuna papa mmoja
1784045511316.png
 
Actually sio wasukuma, makabila mengi sana wamechukulia sherehe/ndoa ni sehemu ya kupiga pesa za wanamichango.

Ni nadra sana kuona harusi za mwanaume anayefunga ndoa, wazazi wake wanawapa zawadi ya million 200, 100 n.k mara nyingi harusi nyingi zinazotrend zawadi nyingi Huwa ni send-off tu, mara nyingi comment unaziziona kutoka Kwa watu Huwa wanasema ""bwana harusi ajipange"

Kile unachokiona kwenye send off zoote Huwa ni kiini macho, ni utapeli mtupu ndio maana harusi iliyofanyika juzi katoro zawadi ilivyotajwa billion 1, bibi harusi hakuonyesha reaction yoyote, kwasababu alikua anajua sio za kwake.

Wazazi wanaandaa sherehe ya gharama na kuita watu wengi, lengo ni kukusanya pesa nyingi na zawadi ya kwenye kamati huwa hapatiwi bibi harusi ila familia/baba ndio anabaki na hiyo hela, bibi harusi anabaki Hana Kila kitu familia inajilipa hizo pesa za zawadi.

Mshikaji wangu mwaka jana alioa, kwenye send off ya MKE wake alikuepo akasikia zawadi ya kamati ni million 17 akasema maisha si ndio aya? Baada ya harusi anamuuliza Mke wake vipi kuhusu pesa maana anashangaa kuona masufuria tu lakini pesa hazioni, MKE wake akamwambia pesa kabaki nazo baba.

Yaani umelipa mahari laki 8 alafu kirahisi tu MKE wako azawadiwe billion 1 aje nazo kwako?

Mwaka huu Kuna mfanyabiashara alikaribia kufirisika kwenye mitikasi yake hapo mwanza, akaona michongo aieleweki akafanya sherehe kubwa Kwa shemeji yake (Kwa kisingizio cha kwamba amemlea yeye) kukusanya watu wengi, zawadi ya kamati million 24 jamaa ikamboost kurudi mjini.

Msitishike na hizo sherehe hapo bibi harusi anaondoka na vyombo tu.

Hakuna
Mimi kama ndiyo bibi harusi napeleka mtu kwa Pilato. Ushahidi upo. Ohooo!!!
 
Back
Top Bottom