Nina hamu ya kuona hawa watu.vijanaume vinachakachua watoto wa watu kuoa havitaki ss hamna jinsi kuwabambika nazo..tena wamwambia ikiwa na miezi saba kabisaaa!
Kama kweli huo ndio huo kunahitajika elimu ya kutosha!Kama mwanaume ndio mwenye tatizo la uzazi kwa mtindo huo atajuaje? Hadi aje kuhisi ni yeye atakua amejaribu kwa wanawake wangapi? Kwa nini wasitumie njia sahihi? Na hata mwanaume akijua tatizo ni lake atanyamaza asimshirikishe mwenzie. Hiki ni nini?Ni sawa na mwanaume kujipima vvu kwa majibu ya mkewe.Tupo gizani!Pamoja na kuhakikisha kuwa wote mnaweza kuzaa hii pia husaidia kujua kama mnaendana kimaumbile,sio ile baada ya ndoa mwanamke anadai huyu mwanamme simuwezi au mwanamme anadai kwa huyu dada naelea tu.
vijanaume vinachakachua watoto wa watu kuoa havitaki ss hamna jinsi kuwabambika nazo..tena wamwambia ikiwa na miezi saba kabisaaa!
sio kupitwa na wakati tu bali wahusika wote wawili hawakupatiwa malezi sahihi ya wazazi wao wapate kujua kuwa kupata mimba ama kutopata sio msingi wa ndoa. Kwanza ni aibu kubwa kwa wazazi wa pande zote mbili, kwa sababu wamedhihirisha wazi kwamba vijana wao hawakuwa waaminifu wakati wa urafiki wao. Ndio maana kila siku nitazidi kuwahimiza wasomaji wengi kukitafuta na kukisoma kitabu CHA NDOA YANGU, NINGEJUA ili kiwasaidie wengi kujitambua na kuepusha ndoa kuja kuingia katika matatzoMimi naona ni kupitiwa tu, wengi huwa wanaanza kuchakachuana mapema. Kitu kikitik wanakimbilia ndoa. Nyingi huwa inatokea bahati mbaya!
Nijuavyo hakuna mwanamke anaeolewa akiwa bokra nowadays especially wanawake wa mjini.wakati wauchumba ni lazma mdonyoane hasa mkiwa mnampango wakuoana,ikitokea ndio mshapima HIV basi ni nyama kwa nyama kwakwenda front huku mkifarijiana kwamba endapo utapata mimba tutaona.
Sababu ya kuoana mtu mjamzito ni kweli sbb ni hiyo mimba ili mtoto asizaliwe nje ya ndoa,hasa upande wa mwanamke huwa wanaforce ili isiwe aibu kwao.Kwakufanya hivi maana halisi ya ndoa inapoteaa kwani mnaweza kuoana wakati bado hamjafahamiana vyakutosha,licha ya mtoto kuzaliwa ndoa inaingia matatani na mwisho huvunjika.
Ni vizuri kwa wale ambao hamjaoa,ukioa mtu unaempenda kwa dhati ili muishi kwa raha,upendo na amani.