Mkuu
Elli.
Najivunia kusoma darasa na shule moja na wewe. Magamba boys haikutoa wavivu wa kufikiri.
Umeeleza ukweli ambao ni mgumu kukubaliwa na Polisi wenyewe au hata wakubwa wao, umedadavua mifano ambayo kila aliye wahi kuwa mikononi mwa Polisi anaijua na kuilewa vizuri kadhia iliyo wahi kuwa mbele yake.
Kwa kweli kama tunahitaji kuwa na jeshi la Polisi bora na lenye tija ambalo wananchi watakuwa na imani nalo angalau kwa 90% lazima tukubali kulifanyia mnyumbuliko wa hali ya juu, kuna haja ya kufumua mfumo wa kuwapata vijana wanao ingia kwenye mafunzo ya uaskari kwa kuwa na vetting nzuri, sifa bora na mafunzo bora kuliko ilivyo sasa.
Nimependa moyo wako wa kutaka kujitolea kuandika training mannual kwa ajili ya mafunzo. Amini nakuambia, mafunzo wanayo pata polisi wetu niya kutumia nguvu zaidi kuliko akili, hawa jamaa huwa hawana muda wa kufikiri kwa usahihi na kutenda kwa usahihi wanapo kutana na chaangamoto ya mhemuko wa raia mbele yao. Hapa na mimi nitakuunga mkono, naweza andaa Training mannual ya "Approach and critical questioning".
Hii inaweza kuwasaidia kwenye utendaji wao wa kila siku tofauti na ilivyo sasa ambapo Polisi wanaamini kumtesa mtuhumiwa ili waupate ukweli, polisi wanaamini kutumia nguvu hata pasipo paswa kutumia nguvu, polisi wanaamini kuua au kujeruhi kwa amri ya mkubwa ndio cheo kipande.
Lazima tufanye mabadiliko makubwa ya mfumo wa jeshi letu, hawawezi kujihubiri kuwa wao ni wana usalama wakati kila siku wanazalisha uhasama na raia.