Hii ndio "Status" ya Jeshi la Polisi kwa sasa

Inawezekana kabisa kuwafanyia Usaili,wa-Kenya wameweza.Cha muhimu tui-ingize katika sheria Mama [KATIBA].
 
Mkuu Elli.
Najivunia kusoma darasa na shule moja na wewe. Magamba boys haikutoa wavivu wa kufikiri.

Umeeleza ukweli ambao ni mgumu kukubaliwa na Polisi wenyewe au hata wakubwa wao, umedadavua mifano ambayo kila aliye wahi kuwa mikononi mwa Polisi anaijua na kuilewa vizuri kadhia iliyo wahi kuwa mbele yake.

Kwa kweli kama tunahitaji kuwa na jeshi la Polisi bora na lenye tija ambalo wananchi watakuwa na imani nalo angalau kwa 90% lazima tukubali kulifanyia mnyumbuliko wa hali ya juu, kuna haja ya kufumua mfumo wa kuwapata vijana wanao ingia kwenye mafunzo ya uaskari kwa kuwa na vetting nzuri, sifa bora na mafunzo bora kuliko ilivyo sasa.

Nimependa moyo wako wa kutaka kujitolea kuandika training mannual kwa ajili ya mafunzo. Amini nakuambia, mafunzo wanayo pata polisi wetu niya kutumia nguvu zaidi kuliko akili, hawa jamaa huwa hawana muda wa kufikiri kwa usahihi na kutenda kwa usahihi wanapo kutana na chaangamoto ya mhemuko wa raia mbele yao. Hapa na mimi nitakuunga mkono, naweza andaa Training mannual ya "Approach and critical questioning".

Hii inaweza kuwasaidia kwenye utendaji wao wa kila siku tofauti na ilivyo sasa ambapo Polisi wanaamini kumtesa mtuhumiwa ili waupate ukweli, polisi wanaamini kutumia nguvu hata pasipo paswa kutumia nguvu, polisi wanaamini kuua au kujeruhi kwa amri ya mkubwa ndio cheo kipande.

Lazima tufanye mabadiliko makubwa ya mfumo wa jeshi letu, hawawezi kujihubiri kuwa wao ni wana usalama wakati kila siku wanazalisha uhasama na raia.
 
Last edited by a moderator:
Kaka niko pamoja sana na wewe, ngoja mwenye kusikia na askie na mwenye kuelewa na aelewe
 
 
Tatizo linaanzia pale polisi wanapotoka depo kwenda kwenye vituo vya kazi; wakati huo polisi hao wapya wanakuwa hawajaanza kupokea mshahara kwa kile kiachoitwa wanaandaa taratibu za malipo ambazo kuna wakati miezi mitatu inapita bila ya hawa polisi wapya kuanza kupokea mishahara.Hivyo njia lahisi kwa wakuu wa vituo huwa wanawapangia vijana hao wapya dolia kila siku ili waweze kukamata watu hovyo mitaani kwaajili ya kujipatia rushwa ili waweze kujikimu.kuthibitisha hilo,angalia wakati depo mpya ya askari wanapoingia mijini huwa ni karaha saana,watu wanakamatwa hovyo.Sasa hapo ndipo tabia ya kupenda rushwa inap[ojengeka hadi inafikia askari rushwa anaiona kama ni haki yake vile
 
Iko valid kabisa naifananisha na bibilia iliyoandikwa miaka mingi lakini kama imeandikwa leo kwa yanayoendelea duniani. Asante kwa kuigusia tena wageni wajionee
 
Iko valid kabisa naifananisha na bibilia iliyoandikwa miaka mingi lakini kama imeandikwa leo kwa yanayoendelea duniani. Asante kwa kuigusia tena wageni wajionee
asante sana sana kwa good remark. Natamani watu wengi wangesoma hapa
 
Mimi nadhani wafanye restructuring ya jeshi hili upya. Kila mkoa wapewe jeshi lao la polisi kama ilivyo marekani. Yaani Dar es salaam Police Department, Mwanza PD
Hii itasaidia sana kupunguza haya yatokeayo leo.
Kila kitengo wachukue watu wanaofaa na sio kama ilivyo sasa.
Wapewe uniform zao pamoja na makoti yanayoonesha wao ni DarPD, wale wa crime scene wapewe zao pia etc.
Hata wale wa madawa ya kulevya, sababu Dar ndio hub kubwa ya madawa iundwe department yao na iwe open na wawe na uniform zao.
Wapewe training upya jinsi ya kudeal na wahalifu etc, wafundishwe pia sheria zao, za wahalifu pia.
 
i wish wangesoma hii kitu hapa
 

Umenena kwa hawa Form 4 Failure na Standard 7, ila ukimwona Policcm aliyesoma ujue ame resit siyo chini ya mara 3 ndiyo akaendelea na masomo, pia hili lina changia sana kwa maana wana low level of thinking capacity.
Leo mtu huyu anapewa DHAMANA YA KULINDA RAIA NA MALI ZAO unategemea atafanya nini?

Ndiyo maana kila mara wanapofanya UTUMBO FLANI wanasingizia tumepewa Order kutoka JUU, na kusahau wao si Maroboti wa kusetiwa. They should think before act, sasa basi kutokana na LOW LEVEL OF THINKING CAPACITY ndiyo maana wanatenda bila kufikiri mara nyingi sana.

Mimi nadhani pia katika Sector hii ya ULINZI NA USALAMA na Sector ya Elimu VILAZA WASIWE NA NAFASI, WAPELEKWE KWENYE PHYSICAL LABOUR.


 

Ongeza:

MAUAJI YA KULIPWA!
Mara nyingi poliCCM hukodiwa na kuahidiwa kulipwa mamilioni ya pesa za mlipakodi/mwananchi/mlalahoi kwa ajili ya kuua raia wasiokuwa na hatia. Hii ni kazi inayofanywa kwa makusudi kwa lengo la kuwadhoofisha UKAWA. Jisomee mwenyewe:
http://www.mwananchi.co.tz/hab...
 

The problem is, is it possible?
 
Mpwa Elli hii topic inabidi iwe sticky.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…