Hii ndio "THE NEW NORMAL" katika jamii zetu kwa sasa.

Hii ndio "THE NEW NORMAL" katika jamii zetu kwa sasa.

Hapo ukimuuliza Sergio ni nini hata haelewi manina! Na anaenda mbali kusema waziwazi mtoto anayeitwa kwa jina la Kiswahili au kilugha jina lake baya!
Wabongo uhususani wanaoishi mijini na hasa wanawake, wana shobo za kipuuzi sana na tamaduni za wazungu, yaan chochote kinachohusiana na asili yao wanaona ni cha kishamba na wanakipuuza ila cha mzungu ndio cha kuiga..

Ukija kwenye suala la majina kwa miaka hii ndio utaona jinsi walivyo kuwa na akili ndogo na ni malimbukeni kweli wa kushobokea majina ya kizungu bila hata kujua maana yake...

Siku hizi ukienda kwenye hivi viday care centers ukiona majina wanayoitwa watoto utacheka, sijui Jayden,Olivia,Charlotte,Ariana.. sijui Grayson mara Daniela, mara Adrian mara sijui yule anaitwa Annabella.

Yaani unaweza kufikiri hao watoto sio watanzania, unaweza ukajihisi labda umetembelea somewhere in London, kumbe uko Tabata mawenzi na shule yenyewe hii uweze kufika lazima uvuke maji machafu yaliyotwama barabarani kwa muda wa wiki mbili.

Mimi ninawakubali sana wasauzi na wanaijeria wanajua sana kuithamini asili yao.

Wasauzi hasa weusi licha ya kuishi na wazungu kwa zaidi ya miaka 400, lakini bado wamestick na tamaduni zao, ukiskia majina yao utakuta ni Andile,Jabulan,Sithole,Buhle,Sibhale,Dlamin...

Vile vile pia kwa wanaijeria, mnaijeria hata azaliwe Los Angeles utakuta anaitwa Chibuzo,Ekenedelichukwu,Obafemi,Kingsley,Nneoma,Oluwafemi.

Kwa mfano sasa hivi kiongozi wa chama cha Consertive party pale UK ni mwana dada mwenye asili ya Nigeria mzaliwa wa London ila jina lake ni Olukemi Olufunto Adegoka Danedoch.

Sasa mbongo hata akizaliwa hapo Masaki tu utakuta anaitwa Henrick Davidson au Alice Johnson.

Yaani wabongo ni malimbukeni na washamba sana ila hawajijui kuwa wao ni washamba.
 
Back
Top Bottom